Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 19 June 2017

MKURUGENZI WA HAMIDU CITY PARK AFUTURISHA KIGAMBONI

HAM1
Hamidu H. Mvungi miliki wa kijiji cha Hamidu City Park, Mikwambe Kibada Kigamboni chenye nyumba 1500 akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari aliyowaandalia wageni wake wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh .Hashim Mgandilwa ambapo aliwashukuru wageni waalikwa hao kwa kujumuika naye katika futari hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, huku akiwatambulisha makazi hayo yenye nyumba za kuuza ambapo ameshirikiana na mabenki mbalimbali na kukopesha kwa watu wanaohitaji nyumba katika kijiji hicho.
HAM02
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa akimshukuru Hamodu H. Mvungi mara baada ya kushiriki katika futari hiyo pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria.
HAM4
Mtangazaji wa Chanel Ten na MC wa Shughuli hiyo ya Futari, Albert Kilala akikaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo.
HAM5
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa na Mwenyeji wake Hamidu Mvungi wakiongoza wageni waalikwa katika futari hiyo.
HAM6 HAM7
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo wakichukua chakula.
HAM8 HAM9
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa katikati , Mwenyeji wake Bw. Hamidu Mvungi pamoja na wageni wake wakipata futari.
HAM10
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando pamoja na wageni mbalimbali waalikwa wakishiriki katika futari hiyo iliyoandaliwa na Bw. Hamidu Mvungi nyumbano kwake Kigamboni.
HAM11 HAM12 HAM13 HAM14 HAM015
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki katika futari hiyo.
HAM3
Hamidu Mvungi na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni , Hashim Mgandilwa wakiwa katika picha ya pamoja.
HAM15
Hamidu Mvungi na Mkewe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni wao.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment