Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 31 January 2017

NOGESHA UPENDO YA VODACOM YAFIKIA TAMATI


Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya Promosheni ya”Nogesha Upendo”jana jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya washindi  400 wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 1/-kila mmoja na zaidi ya wateja 1200 wamejishindia shilingi laki 1 kila mmoja  kupitia promosheni hiyo iliyofikia tamati jana ambayo iliwawesha wateja wa kampuni hiyo kuzawadiwa dakika za muda wa maongezi, MB za intanenti bure na  fedha taslimu pindi wakijiunga na kifurushi chochote cha mtandao huo,Kushoto ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo,Mosi Nassoro.
 ***************
Promosheni ya ‘Nogesha Upendo’ iliyozinduliwa mwezi uliopita imemalizika leo ambapo imewawezesha
 watumiaji  wengi wa mtandao huo kujishindia fedha taslimu na vifurushi vya muda wa maongezi na intanenti.



Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,amesema kuwa promosheni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kufanikisha lengo lililokusudiwa na kuwapa watumiaji wa mtandao huo zawadi ya kipekee.



“Hadi kufikia sasa  wateja wapatao 400  wameweza kujishindia fedha taslimu shilingi milioni 1/-kila mmoja na wateja zaidi ya 1,200 wamejishindia fedha taslimu shilingi laki 1/-kila mmoja na wapo maelfu ya wateja ambao wamezawadiwa dakika za muda wa maongezi na MB za intanenti bure”.Alisema Nkurlu.



Alisema Vodacom inayo furaha kuona promosheni hii imewezesha maisha ya wateja wake kuwa murua na itaendelea kubuni promosheni nyingine zenye lengo la kubadiilisha maisha ya wateja nahuduma mbalimbali za kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidigitali.



”Tunawashukuru sana wateja wetu wote walioshiriki katika promosheni hii kwa kuendelea kuwa katika familia ya Vodacom na tunawaahidi kuendelea kuwapatia huduma bora wakati wowote na mahali popote.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment