Na mwandishi wetu
Usajili wa mbio
maarufu za Kilimanjaro Marathon sasa utaanznia jijini Dar es Salaam katika
viwanja vya Mlimani City, imefahamika.
Muandaaji mkuu na
muanzilishi wa mbio hizo, John Addison alisema usajili huo utaania Mlimani City
na hii itakuwa mara ya kwanza kwa zoezi hilo kufanyika jIjini Dar es Salaamtangu
kuanzishwa kwa mbio hizo miaka 15 iliyopita.
Alisema usajili
huo utafayika Februari 18 na 19 eneo la kuegesha magari mbele ya mgahawa wa
Grano pembeni ya KFC kuanzia saa nane mchana hado saa mbili usiku. “Tunaamini
watu wengi watajitokeza kwa sababu itakuwa mwishoni mwa wiki,” alisema na
kuongeza kuwa hii itapunguza msongamano wa usajili Mjini Moshi.
Meneja Mkuu wa
Mlimani City, Pastors Mrosso alisema wanajivunia kuwa wabia wa Kilimanjaro Marathon
ambazo kwao ni mbio kubwa na wanaamini watu wengi watajitokeza kujisajili na
pia kutembelea maduka mbalimbali na kupata huduma kutoka Mlimani City.
Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye ni mdhamini mkuu aliwapongeza
waandaaji kwa kuanzisha usajili wa Dar es Salaam na kusema itarahisisha zoezi
zima na kuhakikisha kila mtu anasajiliwa kwa wakati na kuepusha msongamano wa
watu siku za mwisho.
Umie Naye
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini, George Lugata aliwataka washiriki wote
watumie fursa hii vizuri ili waweze kushiriki katika mbio hizi.
Kwa mujibu wa Bw.
Addison, Usajili Arusha utafanyika Kibo Palace Hotel Februari 21 na 22 kuanzia
saa nane mchana hadi saa mbili usikuna Moshi usajili utafanyika Keys Hotel Februari 23 (saa sita mchana hadi saa kumi na
moja jioni), Februari 24 (saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni) na Februari 25 (saa
tatu asubuhi hadi saa sita mchana).
“Tumeongeza siku
za usajili kwa vituo vyote ili watu wengi zaidi watumie fursa hii na kuepusha
msongamano wa watu Mjini Moshi tunawaomba washiriki wote watambue kuwa safari
hii usajili utafungwa mapema kabisa kwani hakuna usajili utaendelea baada ya
saa sita mchana Februari 25,” alisema Bw. Addison.
Wadhamini
wa mbio za mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo 21km, GAPCO 10 km-walemavu, Grand Malt-5km. Wengine ni KK Security,
TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair,
Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.
Mbio za mwaka huu
zitafanyika Februari 26 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment