Tuesday, January 17, 2017
|
Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiongoza kikao cha wadau wa kutafuta
suluhu ya mgogoro wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo
uliofanyika Kijiji cha Wasso ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa aliyotoa katika ziara yake hivi karibuni mkoani
humo.
|
Mbunge
wa Jimbo la Ngorongoro ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na
maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akizungumza katika mkutano huo
,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Mwenyekiti wa CCM
mkoa,Lekule Michael Laizer.
|
Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akipokea nyalaka kutoka kwa Mkazi wa
Kijiji cha Wasso ,Tina Timan zilizowahi kutumika kutafuta suluhu ya
mgogoro huo ambao eneo la Kilometa za mraba 1,500 lilitengwa kwaajili
ya kuruhusu shughuli za uhifadhi ya wanyapori jambo linalopingwa na
wenyeji.
|
Afisa
Ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Kasema Samawa akifafanua
namna wilaya hiyo ilivyopanga matumizi bora ya ardhi.
|
Diwani
wa Viti Maalumu katika halmashari ya wilaya ya Ngorongoro,Kijoolu
Kakeya akizungumza kwenye kikao kilichowakusanya wadau wote kujadili
namna ya kupata suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo mkoa wa
Arusha.
|
Mkazi wa Arash ,Rafael Long’oi akizungumzia namna anavyoufahamu mgogoro huo na namna ya kuumaliza kwa njia ya mazungumzo.
|
|
|
|
|
|
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment