Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na Mshauri wa Kitengo
cha Utafiti wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BICO,UDSM), Dk.
Dalmas Nyaoro, baada ya kuwasili eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya
Askari Magereza ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira, akisaini dafrari la wageni baada ya kuwasili
kwenye Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza unaoendelea katika eneo la Ukonga,
jijini Dar es Salaam. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300
ukikamilika.
Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Julius Chego (kulia), akimpa maelekezo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi
huo katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi
watumishi zaidi ya 300 ukikamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi
wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego (kulia) wakati
alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi
huo ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo
la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dk. Juma Malewa
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
Dk. Juma Malewa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), wakati Katibu Mkuu
alipotembelea kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya
Askari wa Jeshi la Magereza, ambao
unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu
Mkuu wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Julius Chego.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa
Kaunda suti), akiteta jambo na Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
Dk. Juma Malewa wakati alipotembelea
kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi
la Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi
watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. (Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment