Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Mohamed Chande Othman
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Juma
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 17 Januari, 2017
amemteua Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Jaji Prof.
Ibrahim Juma anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman ambaye
amestaafu.
Kabla ya kuteuliwa
kushika nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma
alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Mhe. Jaji Prof.
Ibrahim Juma atakaimu nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania mpaka hapo Mhe. Rais
Magufuli atakapofanya uteuzi wa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Uteuzi wa Mhe.
Jaji Prof. Ibrahim Juma unaanza mara moja.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment