Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 13 January 2018

RAIS MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUPUUZA MJADALA WA KUONGEZA KIPINDI CHA URAIS

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole akizungumza mara bada ya kikao chake na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais,  Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
***************
RAIS na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 13, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo, Polepole amesema Dkt. Magufuli amemuelekeza kuwajulisha wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kuwa anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu kuongezwa kwa kipindi cha Urais kutoka miaka 5 iliyowekwa kwa mujibu wa katiba, hadi miaka 7.

Polepole amesema Dkt. Magufuli amewataka wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kwa ujumla kuupuuza mjadala huo kwa kuwa haujawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama, na ni kinyume na katiba ya CCM na katiba ya nchi.

Ameongeza kuwa, Dkt. Magufuli amewataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Polepole amebainisha kuwa Dkt. Magufuli hana mpango wowote na hatarajii kuongeza kipindi cha Urais wakati wote wa uongozi wake.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment