Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 31 October 2017

RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

 Miongoni mwa mabasi 10 chakavu yanatoka kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 za Serikali.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akigua magari yanayotakiwa kukarabatiwa.
 Makonda akikagua basi la Jeshi 
 Basi la Magereza kwa ndani
 Makonda akijaribu kuendesha basi la Magereza
 Basi la Polisi ambalo nalo litafanyiwa ukarabati
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach Ltd kwaajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 za Serikali.

Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach ltd kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.

Makonda amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya Makonda.

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.

Katika hatua nyingine amewataka Wanasiasa kufanya Sasa za kistaarabu badala ya kutukana na kutoa lugha chafu kwa Serikali.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal Rajabu Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza, Noel James, ambapo wote kwa pamoja wamempongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment