Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola akishiriki katika uzinduzi wa operesheni maalumu ya usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Kangi Lugola akizungumza na wanahabari wakati akishiriki katika uzinduzi wa operesheni maalumu ya usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar es Salaam.
usafishaji wa mitaro likiendelea katika eneo la Tandale kwa Ali Maua, maeneo hayo yameathirika kwa kiasi kikubwa na mvua za hivi karibuni kutokana na kurundikana kwa taka ngumu.
TAMKO LA MHE. KANGI ALPHAXARD LUGOLA.
(Mb.) NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MUUNGANO NA MAZINGIRA JUU YA
OPERESHENI MAALUMU IJULIKANAYO KWA JINA
LA "TUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA -TUSALIMIKE"ALILOLITOA KATIKA ENEO LA TANDALE KWA MTOGOLE WILAYA YA KINONDONI
DAR ES SALAAM, 30/10/2017
Harakati
mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuweka Majiji, Halmashauri na Miji, yetu
safi, ikiwa ni pamoja na matamko
mbalimbali ya viongozi wakuu hapa nchini. Aidha, Halmashauri za miji na majiji
zimekuwa zikiendesha kampeni za usafi kwa kuweka siku maalumu za kufanya usafi
wa mazingira na pia kusimamia sheria, kanuni, miongozo na sheria ndogo izinayohusu
mazingira.
Nguvu za ziada zinahitajika ili Halmashauri ziweze kuchukua hatua za dhati
za kudhibiti taka pamoja na kuhakikisha sheria ndogo na sheria nyingine
zinatekelezwa kwa vitendo ili kuhakikisha usafi wa mazingira unasimamiwa
ipasanyo na kuhakikisha mazingira yanayotuzunguka yanakuwa masafi.
Pamoja na kuwepo
kwa sheria mbalimbali bado usafi wa mazingira hauridhishi, taka ngumu katika maeneo mbalimbali kama maeneo
ya makazi na maeneo ya biashara hazizolewi kwa wakati, utunzaji wa mifereji ya
maji ya mvua na utunzaji wa bustani za burudani haujafikia kiwango
kinachostahili, taka bado zinatupwa ovyo kando kando ya barabara na chini ya
madaraja na pia taka kutumika kama njia ya kuziba makorongo na kuzuia
mmomonyoko wa kingo za mito katika makazi ya watu. Tabia hii imesababisha
kuziba kwa mifareji iliyotengenezwa kwa gharama kubwa wakati wa mvua na kusababisha
mafuriko ambayo yamepelekea nyumba nyingi kujaa maji na kuharibu mali za
wananchi na hata kusababisha vifo.
Katika
kuhakikisha kuwa suala la kampeni ya usafi ni endelevu na yenye mafanikio, leo
nataka tuzindue operation maalumu ya kuzibua mitaro yote nchini, operation hii itakuwa endelevu kwa kila
Mkoa, Wilaya , Halmashauri, Kata, Mtaa, Kijiji na Kitongoji. Tutahakikisha kuwa
watendaji wote kulingana na sheria ya mazingira na kamati zao wanahakikisha
kuwa uchafunzi wa mazingira sasa basi. Hatuwezi kuona nchi inaendelea kuwa
katika hali ya uchafu wa aina hii,
wananchi wanakufa kwa kipindupindu na magonjwa mengine wakati watendaji
wapo katika ngazi zote kwa mujibu wa sheria.
Operation hii itakuwa ya
miezi miwili kuanzia tarehe 1 Novemba hadi tarehe 30 Desemba 2017 na haiondoi maelekezo ya awali ya kufanya
usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Baada ya tahere 30 Desemba
2017 ukaguzi wa utekelezaji wa agizo hilii utafanyika nchi nzima kuanzia Januari
2018 Operation hii tutaisimamia sisi
ndani ya Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Maafisa mazingira wa Mikoa
na Wilaya pamoja na watendaji wote hadi
katika ngazi ya kitongoji na kila mtu atawajibika kwa nafasi yake.
Asanteni kwa
kunisikiliza
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment