Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),Elias Kwandikwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akitoa taarifa ya
mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa
kiwango cha lami, mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey
Mwamri,
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akitoa
maelekezo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo
KM 28 kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwamri,
Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akifurahi jambo na
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara
ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa
(Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara zote zenye kipaumbele
katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi kwenye mpango wa
matengenezo.
Kwandikwa ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.
"Unakuta diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa", amesema Mhe. Kwandikwa.

Amesisitiza
kuwa umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo kutambulika
na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa kuwa zitaingizwa
katika mipango ya ujenzi kwa wakati.
Kuhusu barabara hiyo ya Kaliua-Urambo inayojengwa kufuatia agizo la Rais Dkt John Magufuli, Mhe. Kwandikwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora uliopangwa kwa mujibu wa mkataba wake.

"Lengo la
mheshimiwa rais ni kurahisha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi
hivyo mkandarasi huna budi kufanya kazi hii haraka na kw kuzingatia makubaliano
ya mkataba wako.Amesema waziri kwandika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwamnri, amemuhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa serikali ya mkoa huo imejipanga kushirikiana na mkandarasi ili barabara hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.

“Kwanza sisi kama mkoa tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kutuwekea lami katika barabara hii kwa sababu itaongeza ufanisi kwa wananchi kufanya shughuli zao kiurahisi”, amesema Mwanri.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze amesema kuwa Wakala utawasimamia makandarasi wazawa Samota Construction, Anam Roads Works na Jossam Contractor (JV) ili kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo kwa wakati baada ya changamoto ya tatizo la maji kupatiwa ufumbuzi.
Naibu Waziri Mhe. Elias Kwandikwa, yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment