Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 19 October 2017

KATIBU MKUU CHAMA CHA ACT WAZALENDO AJIVUA UANACHAMA NA KUHAMIA CCM

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba (katikati) akitangaza kujivua uanachama na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo. Wengine ni aliyekuwa Ofisa Sheria na Katiba wa Chama Taifa, Mwantumu Mgonja na aliyekuwa Katibu wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Arusha, Wilson Laizer.
*******************
Katika Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba amejivua rasmi uanachama wa chama hicho na kutangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kile alichokidai kuchoshwa na viongozi wa upinzani ambao hawapendi maendeleo yanayofanywa na serikali. Anaripoti Katuma Masamba.

Mwigamba amejivua uanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na wanachama wengine 10 ambao wana nyadhifa mbalimbali Kitaifa na ngazi za Mikoa, huku idadi hiyo ikielezwa kuwa inaweza kuongezeka kulingana na kwamba kwa sasa CCM inatekeleza misingi ya kuhudumia wananchi.

Akizungumza na wanahabari leo, Mwigamba amesema, ameamua yeye na wenzake wameamua kujiunga na CCM ili kuendelea na mapambano ya kurudisha nchi katika kisingi yake kama ilivyokuwa misingi ya chama cha ACT-Wazalendo.

“Tumeamua kujiunga na CCM ili kuendelea na mapambano ya kuirudisha nchi yetu katika misingi yake, lakini pia kujiunga kwetu ni ili kukomesha ufisadi na rushwa,” amesema Mwigamba.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment