Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 30 October 2017

BREAKING NEWS: NYALANDU AJIUZULU UBUNGE

Na Mroki Mroki
MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu ametangaza kujiuzu nafasi zake zote za uongozi ndani ya CCM.

Akitangaza uamuzi huo jijini Arusha leo, Nyalandu amesema amemuandikia barua Spika wa Bunge wa Job Ndugai kumweleza adhma yake ya kujivua nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini.

“Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017,” amesema Nyalandu.


Nyalandu ametoa sababu mbalimbali za kujiuzu kwake nafasi hiyo na kusema kuwa anaondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, akiwa amekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment