Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 13 August 2017

SARAH CHAO AWATIKISA WANAUME UCHAGUZI MKUU WA TFF

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Moira wa Miguu Tanzania, Sarah Chao akila kiapo mbele ya Msajili wa Vyama vya Michezo nchini,Ibrahim Sapi Mkwawa huku akishuhudiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja./Picha:Mroki Mroki.

Sarah aligombea nafasi ya Ujumbe huku akiwa mwanamke pekee aliyejitosa kuwania nafasi hiyo upande wa wanawake na kufanikiwa kuwapiga mweleka wapinzani wake wawili ambao ni wanaume kwenye  Kanda namba 4 yenye mikoa ya Arusha na Manyara na kushinda kwa kupata kura 57 dhidi ya Omar Walii  na Peter Temu waliopata kura 32 kila mmoja.

Baada ya kuapishwa, Chao alisema kuwa anajisikia faraja kuwa mshindi na kwamba ataenda kufanya kazi kwaajili ya maendeleo ya Arusha na Manyara lakini kwa taifa pia.

Alisema, “Ni faraja na ni ushindi wa heshima kwangu. Nitapambana na nitafanya kazi kwaajili ya maendeleo ya soka letu."
Wajumbe mbalimbali wakila kiapo cha maadili mbele ya Msajili wa Vyama vya Michezo nchini,Ibrahim Sapi Mkwawa huku akishuhudiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja.
 ****************
Kwa upande wa Wajumbe walioshinda ni kama ifuatayo; Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: Saloum Chama,  Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza  ni Vedastus Lufano,  Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) ni Mbasha Matutu.  Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) mshindi alikuwa Sarah Chao wakati Katika Kanda namba 5 inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora aliyeshinda ni Issa Bukuku.

Pia  Kenneth Pesambili alishinda kwa upande wa  Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa wakati kwenye Kanda namba 7 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa mshindi alikuwa ni Elias Mwanjali.

Kanda namba 8 yenye mikoa ya Njombe na Ruvuma aliyeibuka mshindi alikuwa ni James Mhagama, Kanda namba 9 Lindi na Mtwara alishinda Dunstan Mkundi wakati Kanda namba 10 yenye mikoa ya Dodoma na Singida aliyeshinda ni Mohamed Aden.

Kanda namba 11, mikoa ya Pwani na Morogoro mshindi alikuwa Francis Ndulane wakati Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga mshindi alikuwa Khalid Mohamed. Kanda iliyokuwa na ushindani mkubwa zaidi ya ni Kanda namba 13 yenye mkoa Dar es Salaam ambapo aliyeibuka mshindi kwa kuwabwaga wapinzani wake 11 ni Lameck Nyambaya.

RAIS WA TFF : Wallace Karia 
MAKAMU WA RAIS : Michael Wambura

WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI
Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment