Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 8 August 2017

MAJI SASA KUUNGANISHWA KWA NJIA YA SIMU

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akifafanua jambo kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa mawasiliano katika simu za mikononi inayowawezesha kupata taarifa zote muhimu za shirika hil kwenye simu. Pamoja naye ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro.
KATIKA kuhakikisha inarahisisha upatikanaji wa  huduma ya majisafi na kwenda na mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kiteknolojia, Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezindua mfumo mpya wa mawasiliano ambao unalenga kumrahisishia mteja kupata na kutoa taarifa zinazohusu huduma hiyo kwa haraka zaidi.

Huduma hiyo mpya sasa itapatikana kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) wa DAWASCO, Kiula Kingu amesema lengo kuu la mfumo huu ni kumweka mteja karibu kihuduma na kila mwananchi ana uwezo wa kutumia mfumo huo katika simu yake kupitia mitandao yote ya simu za mikononi nchini.

Kingu ameongeza kuwa ili mteja kunufaika na mfumo huu anatakiwa kuhakikisha ana simu ya mkononi ya “Smartphone” ambayo itamwezesha kupakua mfumo huo mpya wa DAWASCO, kisha kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajili mteja atatumiwa neno la siri ambalo litamwezesha kuingia na kupata taarifa husika. “Sisi Dawasco tumeona haja ya kujiboresha na kwenda sawa na teknolojia kwa kumletea mteja wetu mfumo rahisi ambao utamwezesha kupata taarifa zetu kupitia simu yake ya mkononi muda wowote,”alisema Bw. Kingu.

Naye, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji  ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.

“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Lyaro.

Anasema kwa sasa wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO itatumia taarifa hizo kumtafuta mteja na kukamilisha taratibu nyingine hadi kuhakikisha mteja anapata huduma ya maji.

 Katika kutimiza agizo la Waziri wa Maji na Imwagiliaji, Mhandisi Greyson Lwengwe la kuhakikisha wakazi wa Dar es salaama, Miji ya Kibaha na Bagamoyo wanapata  huduma ya maji safi, DAWASCO imekua ikijitahidi kuwafikia wananchi kwa njia na mbinu tofauti, kampeni tofauti kama 'mama tua ndoo ya maji kichwani' huku maunganisho ya maji kwa mkopo yakisaidia upatikanaji na uboreshaji wa huduma ya maji kwa maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam.

Mpaka sasa takribani watumiaji 25,000 wa mitandao ya simu jijini Dar es Salaam wameshapakua mfumo huu na lengo la DAWASCO ni kuwafikia wakazi wengi zaidi kwa kipindi kifupi. 


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment