Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL) imewataka Watanzania kuwa
wazalendo na kutumia huduma za mtandao huo ikiwemo huduma ya TTCL Pesa
iliyoanzishwa mwaka huu.
Mtunza fedha Fedha wa Idara ya TTCL Pesa, Liliane Hosea (pichani) ametoa
kauli hiyo katika maonesha ya 41 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika
viwanja vya Julius Nyerere, barabara ya Kilwa.
"Kupitia TTCL Pesa wanaweza kupata huduma mbalimbali za
kutuma na kupokea pesa, pamoja na huduma nyingine za miamala ya kifedha ambayo
mtu anaweza kutumia katika kupata huduma," amesema Liliane.
Aidha, amesema mbali na huduma hiyo lakini pia wateja
watakaotembelea banda lao wanaweza kupata huduma zingine mbalimbali ikiwa ni
pamoja na simu za kisasa, vifaa vya intaneti pamoja na intaneti ya kasi ya 4G.
Naye, Rashid Majid ambaye ni Ofisa Bidhaa wa TTCL amesema,
katika maonesho hayo wana simu za mezani za kisasa pamoja na vifaa vingine ikiwemo
kamera za usalama.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment