Sikiliza video hii
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewataka wanafamilia wa mchezo wa soka
nchini kuwa na subira, kwakuwa Kamati ya uchaguzi mkuu wa shirikisho imeundwa
upya na kilichobaki ni Mwenyekiti wake, Revocatus Kuuli kuwaita wajumbe wa
kamati hiyo.
Msemaji
wa shirikisho hilo, Alfred Lucas amesema, tayari kamati hiyo imeshafanyiwa
marekebisho kwa kuondoa baadhi ya wajumbe na kuweka wajumbe wengine wapya.
"Mambo
yote yako tayari, wanafamilia wa soka wawe na subira tu, kwasababu wajumbe
wameshateuliwa na kilichobaki ni Mwenyekiti kuwaita, kwahiyo nafikiri ndani ya
siku mbili hizi tutawatangazia mashabiki wa mpira rasmi," amesema Luca.
Lucas
pia amesisitiza kuwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo bado
haijabadilika bali unatarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
Aidha,
amesema kilichosababisha kamati ya kwanza kuvunjwa ni baada ya Kamati ya
Utendaji ya TFF kujidhihirisha kuwepo kwa kutokuheshimiana na uelewa mdogo,
mgongano wa maslahi pamoja na nidhamu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment