Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) limeeleza azma yake ya kuwawezesha
watoto wengi kuwa na bima ya afya, kupitia fao la Toto Afya Kadi inayotolewa
katika maonesho ya Sabasaba. Anaandika Katuma Masamba.
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Hawa Duguza amesema, katika
maonesho hayo watakuwa wakitoa vitambulisho vya bima siku moja baada ya mzazi
kuwasilisha taarifa zote zinazohitajika.
"Tuko hapa kwa ajili ya kutoa elimu na kuhamasisha watu
kujiunga na bima ya afya na hasa fao jipya la Toto Afya Kadi ambayo ni mahususi
kwa watoto," amesema Hawa.
Amesema ili mzazi aweze kupata kadi ya Toto Afya Kadi kwa ajili
ya mtoto wake atalazimika kuwasilisha vivuli vya kadi ya mtoto ya kuzaliwa na
picha ndogo na baada siku moja atapewa kitambulisho cha mtoto wake.
Mbali na hilo amesema, kupitia maonesho hayo wanapokea
malalamiko na changamoto mbalimbali kutoka kwa wateja wao na kuyafanyia kazi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment