Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 25 July 2017

SERIKALI IPO MBIONI KUPELEKA BUNGENI MUSWADA WA SHERIA WA ULINZI BINAFSI ILI KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kupeleka bungeni Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi (Personal Data Protection Act) ili kudhibiti matumizi mabaya ya simu za mkononi, barua pepe na mitandao ya kijamii. Anaandika  Matern Kayera.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani wakati akifungua mkutano wa pamoja kati ya Wachina na Watanznia uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Sheria hiyo ya kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii itakuwa ya tatu baada ya sheria ya uhalifu wa kimtandao (Cybercrime Act) na sheria ya miamala ya kimtandao (Online Act) kupitishwa mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Ngonyani, watumiaji wa simu waliosajili simu zao za mkononi imeongezeka kutoka 300,000 mwaka 2000 hadi kufikia milioni 39 kwa sasa.

Naye Balozi wa China nchini, LU Youqing alisema kwamba matumizi ya mitandao ya kijamii yameimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na China. Alisema ushirikiano kati ya Tanzania na China umekuwa na manufaa katika nyanja mbalimbali kama vile kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, amani na usalama, ushrikiano wa kimataifa na ushirikiano baina ya mtu na mtu.


Kuhusu maendeleo ya inteneti alisema kwamba kati ya makampuni 10 makubwa ya intaneti duniani, makampuni manne yanatoka China. Alisema matumizi ya intaneti nchini Tanzania nayo yanakuwa kwa kasi kwani kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), watumiaji wa simu za mkononi waliosajiliwa  imeongezeka mara 13.7 zaidi kwa kipindi cha miaka 10 kutoka watu milioni 2.9 mwaka 2005 hadi kufikia watu milioni 39.8 mwaka 2015.


“Watumiaji wa mitandao nao wameongezeka mara 17 zaidi kutoka milioni 1.01 mwaka 2005 hadi kufikia milioni 17.26 mwaka 2015,” allisema Balozi LU Youging na kuongeza kuwa


“China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara na wa pili kwa uwekezaji Tanzania. Uwekezaji wa China nchini Tanzania umefikia dola za Marekani bilioni 7.” 


Alileza kuwa ushirikiano katia ya nchi hizi mbili umeweza kutengeneza ajira zipatazo 200,000 kwa Watanzania na zaidi ya Watanzania 350,000 wanajishughulisha na biashara kati ya China na Tanzania.

 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim Yonazi akitoa mada katika mkutano huo.
 Washiriki kutoka sehemu mbalimbali vikiwepo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, watoa huduma za simu na vyombo vya ulinzi wakifuatilia majadiliano. Picha na Mroki Mroki. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.

 Naye Balozi wa China nchini, LU Youqing alisema kwamba matumizi ya mitandao ya kijamii yameimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na China.
 Washiriki wakifuatilia mkutano
 Mwogaji wa mkutano huo, Innocent Mungy akiwajibika
 Mijadala iliendelea ...
 Baadhi ya watoa mada wakisikiliza kwa umakini

Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Annastazia James Wambura akizungumza wakati wa ufungaji wa Mkutano huo wa siku moja.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Annastazia James Wambura akizungumza jambo na Mhariri mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi.


Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Annastazia James Wambura akifurahia jambo akiwa pamoja na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Rodney Thadeus (kushoto) wakizungumza baada ya kufunga mkutano huo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment