Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 27 July 2017

MAKONDA AGAWA KOPYUTA KATIKA MANIPAA ZA DAR ES SALAAM KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akikabidhi moja ya komopyuta kwa viongozi wa Wilaya na Manspaa za mkoa wa Dar es Salaam ambazo zinalenga kutoa huduma kwa haraka kwa wananchi.
 Watumishi wakichukua Kompyuta hizo hii leo.
KOMPYUTA za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilling Million 170 kwa zimekabidhiwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Manispaa tano za Mkoa huo pamoja na Watu wa Jiji na Mkoa kwaajili ya kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi.

Katika mgawanyo huo kila Manispaa imepatiwa Computer nane huku Ofisi ya Jiji wakipatiwa Computer tano na Ofisi ya Mkoa wakipatiwa Computer tano ikiwa ni ufadhili wa kampun ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono Mheshimiwa Makonda kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri.

Makonda amesema kompyuta hizo zitawekewa Mfumo wa kisasa ujulikanao kama Ardhi E.System utakaoziunganisha idara zote zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi (One stop Center) ili kurahisisha Mwananchi kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi ambapo mwananchi atakuwa na uwezo wa kutuma maombi ya kibali cha ujenzi kwa kutumia simu ya mkononi ke au Computer hata akiwa nyumbani na akapewa majibu yake kwa haraka.

 “Kazi yangu kubwa ni kupunguza mateso,malalamiko na kero za Wananchi dhidi ya kero ya Ardhi, na namna mbili ya kupunguza ni kuwawezesha watendaji kuwa na nyenzo na vifaa vitakavyorahisisha kufanya kazi zao kisasa zaidi kuendana na kasi ya Rais wetu Dr.John Magufuli, namna ya pili ni kusimamia uwajibikaji kwamba kila mmja anatekeleza majukumu yake ili Mwananchi wa Mkoa wa Dar es salaam asipate adha na mateso aliyokuwa akiyapata kwenye Sekta ya Ardhi, umuhimu wa kutoa vibali vya ujenzi ni muhimu katika mji huu unaokuwa kwa kasi barani Afrika” Alisema Makonda.

Aidha kompyuta hizo zitawekewa Mfumo maalumu utakaokuwa ukikusanya Maoni na mapendekezo ya wananchi ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kutuma maoni yao na kero mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta ya Ardhi.

“Tumeishi sana kwenye mfumo wa makaratasi na mafaili, na wakati mwingine kumekuwa na changamoto ya kupotea kwa mafaili na mwananchi kupata adha ya kutoelewa nini afanye maana ataanza upya kutuma maombi, lakini sio hivyo inafanya kazi kuwa ngumu, pia ni chanzo cha rushwa pale mwananchi anapokuwa akisumbuliwa na mtumishi, naamini Compuer hizi zinaenda kukata mzizi wa fitina, Wananchi kulundikana ofisini ni kero kubwa, wananchi kusumbuka kupata huduma ni kero kubwa”, Alisema Makonda.

“Niwaombe watumishi wa Ardhi mtoeni Raisi wenu kimasomaso, mfanyeni ajisikie fahari kufanya kazi na nyie, na namna pekee ya kumpa heshima hii ni kuwatumikia na kuwahudumia vizuri wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwa uaminifu mkubwa na uadilifu, hili linawezekana kwa asilimia mia moja, Aliongeza Makonda.

Hata hivyo ameipongeza Kampuni ya TAMOBA kwa kuamua kunga mkono ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kueleza kuwa Computer hizo zitaenda kufanya kazi iliyokusudiwa ya kupunguza adha kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya TAMOBA Bwana Joseph Kimisha amesema kuwa kampuni yao itaendelea kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Dar es salaam katika masuala mbalimbali ili kuhakikisha wanatatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Katika Makabidhiano hayo pia Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TAMOBA Bwana Otieno Igogo amesema watatoa jumla ya Printer 10 kwaajili ya kusaidia utendaji kwa manispaa za jiji la Dar es salaam ambapo kila manispaa itapata Printer mbili


1 comment: