SERIKALI imetangaza kufuta ada ya
mwaka ya leseni ya magari (Annual Motor Vehicle Licence Fee) iliyokuwa ikilipwa
na na wamiliki wa magari kila mwaka ili ilipwe mara moja wakati gari
linaposajiliwa. Anandika Katuma Masamba-dailynewstzonline.blog
Ada hiyo iliyokuwa ikitozwa kila
mwaka bila kujali kama gari linafanya kazi au limeegeshwa kwa kuwa ni bovu,
sasa italipwa mara moja gari inaposajiliwa na baada ya hapo itaenendelea
kulipwa kupitia ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya petroli, dizeli na taa kwa
kuongeza ushuru kwenye bidhaa hizo.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip
Mpango ameyasema hayo wakati akiwasilisha bajeti kuu ya serikali ya mwaka
2017/18.
"Aidha, serikali inatoa msamaha
wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote (tax Amnesty) ya ada hiyo
yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma," amesema Dk Mpango ambaye alikuwa
akipigiwa makofi na wabunge.
Dk Mpango pia amesema serikali inapendekeza
kuongeza ada ya leseni ya magari wakati wa usajili mara ya kwanza ambapo
ongezeko hilo na kiasi kwenye mabano ni gari yenye ujazo wa injini ya 501 hadi
1500 cc (kutoka Sh 150,000 hadi 200,000), gari la 1501 hadi 2500cc (kutoka Sh 200,000
hadi 250,000).
Gari lenye ujazo wa 2501cc na zaidi
kutoka kiwango cha sasa 250,000 hadi Sh 300,000 na kwamba hatua hizo
zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa Sh milioni 77,603.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment