Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akisoma Bungeni Mjini Dodoma leo Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
**********
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk
Philip Mpango amewaonya watumishi wa Mamlaka ya Mapato tanzania (TRA) kutotumia vitisho na unyanyasaji kwa walipa
kodi, kwa kuwa atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria
za utumishi wa umma. Anandika
Katuma Masamba-dailynewstzonline.blog
"Wale watumishi wa TRA ambao
naamini ni wachache tu, wanaojihusisha na vitendo hivyo, wakome kabosa kufanya
hivyo," amesema Dk Mpango na kushangiliwa na wabunge.
Akiwasilisha bajeti, Dk Mpango
amesema matumizi ya vitisho, unyanyasaji kwa walipakodi, kuwadai rushwa au
kuwazidhishia makadirio ya kodi ili kuwakomoa ni mambo ya hovyo na hayakubaliki
hata kidogo.
Aidha, Dk Mpango ametoa rai kwa
wafanyabiashara na wananchi wazalendo kutoa taarifa za ukweli kuhusu mwenendo
mbaya wa mtumishi yeyote ili zifanyiwe kazi, pia wafanye hivyo katika kutoa
taarifa za wafanyabiashara wanaokwepa kodi ili washughulikiwe ipasavyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment