SERIKALI imepiga marufuku
usafirishaji wa madibni kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi
na badala yake itaanzisha utaratibu ambao utahakikisha inapata mapato halisi. Anandika Katuma Masamba-dailynewstzonline.blog
Badala yake imesema itaanzisha
maeneo maalumu (clearing houses) katika viwanja vya ndege vya kimataifa,
migodini na kadhalika ambapo madini hayo yatapewa kibali cha kusafirisha madini
hayo ambacho kitatozwa ada ya asilimia moja (clearence fee) ya thamani ya
madini hayo.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk,
Philip Mpango akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/2018 amesema hatua hiyo
itasaidia serikali kujua thamani halisi ya madini hayo na kukusanya mapato
stahiki.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment