SERIKALI imeazimia
kusamehe Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) ili
kupunguza gharama za ununuzi na uagizaji mashine na mitambo ya kuzalishia na
hivyo kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda. Anandika Katuma Masamba-dailynewstzonline.blog
Hatua hiyo
, itahusisha viwanda vya mafuta ya kula, nguo, ngozi, dawa cza binadamu na
mifugo. Lengo la kufanya hivyo ni kuvutia wawekezaji katika sekta za viwanda,
kilimo cha mazao na mifugo pia kukuza ajira na kukuza uchumi wa nchi.
"Hatua
hii itawezesha viwanda vidogo na vya kati kupata unafuu wa gharama za kulipa
kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mashine na mitambo watakayonunua kwa ajili ya
kusindika na kutengeneza bidhaa mbalimbali," amesema Waziri wa Fedha na
Mipango, DK Philip Mpango.
Amesema
mitambo na mashine zote zitakazosamehewa kodi ya Ongezeko la Thamani
zitaanishwa kwa kutumia HS Codes.
Aidha, amesema serikali imeondoa kodi ya Ongezeko la
Thamani kwa kiwango katika huduma
zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa na mizigo nje ya nchi (ancillary
transport services).
Kwa mujibu
wa Dk Mpango lengo la hatua hiyo ni kupunguza gharama za usafirishaji katika
bandari za tanzania kwa kuifanya tanzania kuwa njia bora zaidi ya kupitisha
bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwenda nchi nyingine hususan zisizo na bandari
(landlocked countries).
"Hatua
hii itahamasisha wasafirishaji kutoka nchi jirani kupitisha mizigo yao kwa
wingi kwenye bandari zetu na hivyo kukuza uchumi wa nchi kutokana na kuongezeka
kwa mapato ya bandari," amesema Dk Mpango.
Hatua hizi
zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake zinatarajiwa kupunguza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 48,034.1.
Baada ya
waziri mwenye dhamana kuwasilisha bajeti hiyo, wabunge wanatarajiw akuanza
mjadala Juni 12 mwaka huu kuhus mapendekezo au maboresho waliyonayo katika
bajeti hiyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment