Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Holycross, Prisca Muthoni kombe pamoja na cheti kwa shule hiyo kufanya vizuri katika elimu katika Manispaa ya Temeke. Makabidhiano hayo yalifanyika katika siku ya elimu ya Manispaa hiyo. (Picha na Mroki Mroki).
Wapiga ngoma wa Kundi la Tunaweza kutoka Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto Ally Rashidi , Nurdin Bilali na Jotham James wakitoa burudani wakati wa Siku ya Elimu Manispaa ya Temeke iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiimba wimbo maalum wa maadhimisho ya Siku ya Elimu Temeke.
Walimu kutoka Shule mbalimbali za msingi na Sekondari Manispaa ya Temeke wakiwa katika maadhimisho hayo Mei 4,2017.
Wanafunzi wenye ulemavu kutoka kituo cha Jeshi la Wokovu Dar es Salaam wanaounda kundi la Twaweza band wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya elimu Manispaa ya Temeke yaliyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), jana. (Picha na Mroki Mroki). Wapiga ngoma wa Kundi la Tunaweza kutoka Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto Ally Rashidi , Nurdin Bilali na Jotham James wakitoa burudani wakati wa Siku ya Elimu Manispaa ya Temeke iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.
Wanafunzi kutoka Sekondari ya Mbagala wakiigiza kama Askari wa kikoloni katika vita vya Majimaji
IDARA ya Elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke, imeomba kubadilisha baadhi ya shule za msingi ambazo zina wanafunzi
wachache ziwe shule za sekondari kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza elimu ya
msingi kujiunga kidato cha kwanza.
Shule hizo ni Ndalala yenye wanafunzi 332 na
Serengeti yenye wanafunzi 361.
Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Sylvia
Mutasingwa alisema hayo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Elimu yaliyofanyika jijini
Dar es Salaam, ambapo pia walitoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa shule
zilizofanya vizuri pamoja na wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na
kidato cha sita.
Mutasingwa pia aliomba kuwatumia maofisa elimu
kata ili kuwashirikisha wazazi kikamilifu katika suala la maendeleo ya elimu ya
watoto wao.
Katika hatua nyingine, alieleza matatizo
walinayo kuwa ni msongamano wa wanafunzi madarasani ukilinganisha
na idadi ya vyumba vya madarasa vilivyopo.
Vile vile ushirikiano mdogo wa wazazi katika
kupata taarifa za watoto wao kutoka kwa walimu pamoja na wanafunzi
kutokufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao, mahudhurio na hata tabia
za wanafunzi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa
mgeni rasmi Felix Liyaniva, alisema amezipokea changamoto zote pia atashirikiana
na wadau mbalimbali wa elimu katika kuzitafutia ufumbuzi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment