Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi
kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Consolata Ngimbwa akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakandarasi Wanawake mara baada ya kufungua Mkutano wa siku mbili wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.

****************
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa
miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa
kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia
kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati
anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa
Wakandarasi mwa mwaka 2017.
Makamu wa
Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na
sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa
kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio
vinginenevyo.
Makamu wa
Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza
kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya
ujenzi wanayopewa.
Amesema
kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti
kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida
mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira
za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.
“Hatuwezi
kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni
lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”
Kuhusu
madeni ya wakandarasi, Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Wakandarasi kuwa Serikali
haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo
imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha Wakandarasi.
Ameahidi
kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga
mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.
Kwa
upande wake, Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa
Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili
kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.
Waziri
Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi
majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa
wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na
kupewa kazi.
Amesema
kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo
wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.
Nae, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi
Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa
kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa
bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.
Msajili
huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo
ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia
71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo
miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa
wafanyakazi.
Kasoro
nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi
kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment