Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 28 May 2017

AJALI ALIYONUSURIKA JONAS MKUDE YAUA SHABIKI WA SIMBA

 MMOJA wa majeruhi wa gari walilokua wakisafiria mashabiki wa Simba Toyota V8 T834 BLZ ambapo pia nahodha wa mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania, Simba Sc Jonas Mkude alikuwepo, Shose Masao amefariki. Anaandika Mroki Mroki.

Majeruhi wengine waliokua katika gari hilo  akiwepo Mkude, Faudhia Ramadhan na ,Jasmine Mdoe pamoja na dereva na mmiliki wa gari hilo aliyetambulika kama Presidaa wamaendelea vyema.

Taarifa za awali zina sema Mkude alipelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi wa afya yake na yuko vizuri. 

Aidha mwili wa Marehemu Shose unataraji kusafirishwa hadi Hospitali ya Mwananyamala tayari kwa mipango ya mazishi.
TAARIFAyetu ya awali baada ya kitokea ajali iliarifu kuwa Nahodha wa Mabingwa wa kombe la Shirikisho na Kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo, Dumila katika shamba la Mitiki, zinaarifu kuwa hakuna watu wawili ambao bado majina yao hajapatikana wameumia na Mkude kupata majeraha madogo na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

 Watu hao walikuwa katika gari aina ya Toyota VX lenye namba za Usajili T 834BLZ na walikuwa wakitokea Dodoma kushuhudia fainali za kombne la Shirikisho la Soka Tanzania uliopigwa jana katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma uliozikutanisha Simba na Mbao.

Simba ilishinda mchezo huo kwa bao 2-1 na kutwaa ubingwa huo na kujipatoia tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment