Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 27 April 2017

ODINGA APITISHWA NA MUUNGANO WA UPINZANI NASA KUWANIA URAIS KENYA

HATIMAYE Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Omolo Odinga (pichani) kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.
Kwa uteuzi huo Odinga sasa atapanda katika majukwaa ya kampeni kwa mara ya nne akiwania kiti cha Urais wa Kenya na safari hii akikabiliana na Uhuru Kenyatta kutoka cha Jubilee ambaye anatetea nafasi hiyo.
Akizungumza baada ya kupewa nafasi hiyo hii leo Odinga ambaye ni kiongozi wa chama cha ODM amesema kuwa viongozi wa NASA wamempa heshima kubwa kuipeperusha bendera ya chama chao.
"Hii ni heshima kubwa sana ambayo ndugu zangu wamenifanyia, kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA. Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku nyingi. Kila kitu tumeandika, tumekubaliana ya kwanza serikali tutakayoiunda, ambayo ni serikali ya mseto itakuwa ni serikali ya mpito," alisema Odinga.
Aliongeza kwa kusema kuwa "Sisi tuko kama timu, yenye pembe tano (Pentagon), wamenipa utepe wa nahodha, hiyo inaniunganisha mimi nao na Wakenya wote, tutatembea pamoja bega kwa bega. Tunataka kubadilisha Kenya na kutekeleza ndoto ya waanzilishi wa taifa letu".
Muundo wa Serikali ya NASA pindi ikiingia madarakani kuongoza Serikali ya Kenya

Muundo wa Serikali ya NASA umesha wekwa hadharani ambapo Naibu Rais ni Kalonzo Musyoka wakati Waziri Mkuu ni Musalia Mudavad ambaye atasaidiwa na Manaibu Waziri Wakuu wawili ambao ni Moses Wateng'ula ambaye atahusika na Utumishi wa umma na Masuala ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, huku Naibu Waziri Mkuu mwingine akiwa ni Issac Rutto atake husika na masuala ya Utawala na mipango lakini pia masuala ya fedha.

Akielezea vipaumbele vya serikali yake pindi akishika madaraka ya Kuiongoza Kenya kuwa ni kumaliza umasikini, kuimarisha afya, kuboresha uchumi, kubuni nafasi za kazi na kurejesha gharama ya elimu na maisha chini.
Odinga pia ameahidi kuhakikisha walimu na madaktari,pamoja na wafanyakazi wengine wanalipwa mishahara mizuri na kuahidi akishinda serikali yake itamaliza rushwa serikalini.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment