Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 27 April 2017

NANI KATI YA ODINGA,MUSYOKA,MUDAVADI,RUTO NA WETANGULA KUIPEPERUSHA BENDERA YA NASA UCHAGUZI KENYA


Waziri Mkuu wa zamani na Mwanasiasa wa siku nyingi wa Kenya, Raila Amolo Odinga, au maarufu kama anavyojulikana na wafuasi wake kama  Agwambo, Tinga, Baba, RAO au  Jakom, Odinga alikuwa Waziri Mkuu mwaka 2008 to 2013. Endapo atapitishwa na Muungano wa vyama vya upinzani Kenya (NASA) hii leo atakuwa amegombea kwa mara ya nne mfululizo.


Aliyekuwa naibu wa Rais na kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka amejilinganisha na Donald Trump na kuahidi ushindi endapo atagombea uchaguzi ujao. Musyoka alipata kuwa makamu wa Rais wa Kenya chini ya Utawala wa Rais Daniel Arap Moi 2008-2013


Musalia Mudavadi ni kiongozi wa Chama cha Amani National Congress (ANC), na alipata kuwa Makamu wa Rais 2002 na Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Kenya kati ya 2008-2012.

Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) na Gavana wa zamani wa Gomet, Isaac Ruto nae ni mmoja wa wanasiasa wa Kenya walioonisha nia ya dhati kumpoka kiti rais Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula, nae ni moja kati ya Wanachama wa tano wa Nasa wanaowania nafasi ya kuteuliwa kugombea Urais kupitia Muungano huo.
***********

ZIKIWA zimesalia siku 102 kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Rais, Magavana, Seneta, wabunge na madiwani nchini Kenya Muungano wa vyama vya upinzani huenda wakatangaza mgombea wao hii leo.

Muungano huo wa vyama vya upinzani nchini Kenya una watu watano mashuhuri wanaowania kuteuliwa na umoja huo kuchuana na Rais wa sasa wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka huu.

Taarifa kutoka ndani ya muungano wa vyama hivyo vya upinzani nchini humo ujulikanao kama National Super Alliance, yaani NASA, uilisema itatangaza mgombea wake wakati wowote.

Wagombea watano walio ndani ya NASA, ni pamoja na mgombea Urais wa muda mrefu katika chaguzi za Kenya Raila Odinga, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa.

Wanasiasa wengine walio ndani ya Nasa ni pamoja na  Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka, Makamu wa Rais wa zamani Musalia Mudavadi, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Moses Wetangula na Mwenyekiti wa zamani wa baraza la Magavana Isaac Ruto.

Ruto, anayeongoza chama cha Chama cha Mashinani (CCM) alikuwa kwenye muungano wa vyama vinavyomuunga mkono, Uhuru Kenyatta kabla ya kuhama na kuunda chama chake.

Odinga ndiye kiongozi wa chama cha ODM, ambacho kina wabunge wengi zaidi katika Bunge la sasa.

Iwapo atachaguliwa kuwa mwaniaji wa Nasa, basi itakuwa ni mara ya nne kwake yeye kuwania nafasi hiyo bila mafanikio ingawaje anaamini kuwa alishinda uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo Rais wakati huo, Mwai Kibaki alitangazwa mshindi, na kuzua tafrani nchini Kenya ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.

Huku hayo yakijiri, wanasiasa wengi wanaendelea kupoteza viti vyao kwenye kura za maoni.

Wakenya kwenye mtandano wamekuwa wakiendesha kampeni inayoitwa Opresheni Fagia Wote, ambapo baadhi ya maeneo ya uchaguzi yamewawafagia Magavana, Seneta, wabunge na madiwani wote.

Kampeni ya Fagia Wote inapania kuonyesha ghadhabu ya Wakenya kwa jinsi taifa hilo limeendeshwa kwa miaka minne iliyopita. Kumezuka vurugu kwenye sehemu kadhaa nchini na pia madai ya kuiba na kununua kura.

Askofu mmoja wa kike, Margaret Wanjiru ambaye amewahi kuwa waziri, ambaye kwa sasa alikuwa anawania kuwa Gavana mpya wa Nairobi, alilala kwenye seli ya Polisi alipokamatwa jana kwa madai ya kuzua rabsha katika kituo cha uchaguzi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment