Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 14 March 2017

WATANO AKIWEPO MBUNGE MABULA WA NYAMAGANA WANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI MOROGORO

Mmoja wa majeruhi John Dotto Kisute katika ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo Toyota Harrier namba za usajili T 282DKD lililogonagana na trekta T 620AZV huko Wami Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro
 
Na Mroki Mroki
WATU watano akiwepo Mbunge wa jimbo la Nyagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula wamenusurika kifo baada ya kari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kugongana na Trekta usiku wa kuamkia leo.

Kwamujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ilitokea katika eneo la Wami Dakawa, Wilaya ya Mvomero mkoani Mporogoro.

Matei alisema gari hilo lilikuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam na chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa trekta T 620AZV lilolokuwa na tela T634AVS kuingia barabara kuu biloa tahadhari na kuligonga gari T 282DKD Toyota Harrier iliyokuwa ikiendeshwa na Dickson Amosi Byaro.

Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni dereva wa gari hilo, Dickson Byaro mkazi wa Tabata Dar es Salaam, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula mkazi wa Mwanza na Kalala Hamza Kalala mkazi wa Kijitonyama ambao walipatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Majeruhi ambao wamelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Morogorio wakiendelea na matibabu ni John Dotto Kisute mkazi wa Makongo Dar es Salaam na Halidi Mashahi mkazi wa Buhongwa mkoani Mwanza.

Kamanda Matei alisema Jeshi la Polisi bado linamtafuta dereva watrekta ambaye alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment