Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday, 24 March 2017

TOVUTI ZA SERIKALI ZA MIKOA NA HALMASHAURI ZOTE TANZANIA KUWA HEWANI JUMA LIJALO

MAFUNZO ya Maofisa Habari na Maofisa Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Dodoma, Iringa, Singida, Geita, Manyara, Pwani na Dar es Salaam juu ya Utengenezaji na uendeshaji wa Tovuti za Halmashauri na Mikoa unaendelea.

Mafunzo hayo yanatolewa chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3).

Mradi huo wa miaka mitano, na unafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara. Ila katika uboreshaji wa mawasiliano kwa umma mradi huo unashirikisha Halmashauri na mikoa yote ya Tanzania bara kwa kuwapa mafunzo maafisa habari na maafisa Tehama wa maeneo husika.

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
 Washiriki wa Mafunzo hayo ambao ni Maofisa Habari na Tehama kutoka Halmashauri na Mikoa wakiendelea na mafunzo juu ya uingizaji habari na taarifa mbalimbali za maoeneo yao. Endapo Halmashauri zote na mikoa zitafanikiwa kuzifanyia kazi tovuti hizo wananchi katika maeneo mbalimbali watakuwa na uwezo wa kupata taarifa za shughuli za serikali na kuondoa kero ya uwazi katika shughuli za umma.
Mradi huu unataraji kuzinduliwa ngazi ya taifa Machi 27 mwaka huu mjini Dodoma ambapo mikoa na Halmashauri zake zote nchini sasa zitapatikana katika tovuti kwa majina yao. Tayari mikoa ya Kanda ta Ziwa imesha zindua tovuti zao na mikoa mingine iliyosalia uzinduzi utafanyika Jumatatu ijayo.BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.

Wananchi sasa wataweza kuperuzi taarifa za maeneo yao kupitia simu zao za kiganjani pamoja na njia nyingine mbalimbali za mawasiliano ya Intanenti.
 Baadhi ya wakufunzi katika mradi huo wa PS3 wakifuatilia kwa njia ya mtandao kazi zinazofanywa na washiriki wa mafunzo hayo na kuwapa ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
Miongoni mwa vitu ambavyo vinapaswa kufanyika katika tovuti hizo ni kutoa taarifa za shughuli za serikali ngazi ya Halmashauri au Mkoa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na shughuli za miradi ya maendeleo na kuwafikia wananchi kujua kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka na wakati ili kueopusha kuwepo kwa taarifa za uongo mitaani.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment