Na Mroki Mroki, Dodoma
SERIKALI imeagiza Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,
Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi,
Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuachiwa huru.
Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, wakati akiongea na
waandishi wa habari mjini Dodoma na kusema kuwa hata wimbo anaotuhumiwa nao
kuwa umekiuka maadili uendelee kupigwa.
Msanii Ney alikuwa akishikiliwa na Jeshi la
Polisi baada ya kumkamata juzi mkoani Morogoro na kumsafirisha hadi jijini Dar
es Salaam kufuatia amri ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kile
kilichodaiwa ni wimbo huo kukosa maudhui na kukiuka sharia za Basata.
Waziri Mwakyembe alifuatilia sakata hilo la
kukamatwa Ney na baadae Basata kufahamisha sababu za kumkamata na kutakiwa
kuhojiwa juu ya nyimbo yake ya ‘Wapo’ lakini pia Rais alimuagiza kugfuatilia
suala hilo na kuona namna ya kulimaliza kwakuwa haoni kosa katika wimbo huo.
Aidha Mwakweye amesema Rais Magufuli aliomba Ney
achiwe hivyo nayeye akiliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru msanii huyo
“Baada ya kuzungumza na Rais Dk John Magufuli
ambaye yeye binafsi ameonesha wazi kuupenda wimbo huo kutokana na mindundo yake
nimesha BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee
kupigwa tu kama nyimbo nyingine,”alisema Mwakembe.
Waziri Mwakyembe alisema katika mazungumzo yake
na Rais Magufuli alionesha kufurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri
Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile
Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga,
Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.
Pia alisema alichofanya Ney wa Mitego katika
wimbo wake huo ni kutumia Uhuru wa Kujieleza hivyo Rais alisema endapo Mtu
anafanya kitu cha manna hiyo na hajavunja sharia hakuna haja ya kumzuia.
Akizungumza kisheria alisema Basata inamamlaka
ya kufanya ilicho fanya kwakuwa ni eneo lake hata yeye Waziri hawezi kutoa
agizo kwa basata ila anawaomba tu wamwachilie msanii huyo na wimbo wake kuendelea
kupigwa.
Mwakyembe pia amemwomba Msanii Ney wa Mitego
kesho akitane nae mjini Dodoma kwa mazungumzo na kumshauri maeneo ya
kuongeza katika wimbo wake huo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment