Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Uyole mkoani Mbeya. Makalla amewataka watendaji wa serikali katika ngazi
mbalimbali kuzishughulikia na kuzipatia majibu kero za wananchi kwa haraka.
Wananchi Kata ya Uyole wakiuliza maswali kuhusiana na kero zao mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akimsikiliza Kamanda wa Polisi akijibu baadhi ya kero za wananchi.
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewataka watendaji wa serikali katika ngazi
mbalimbali kuzishughulikia na kuzipatia majibu kero za wananchi kwa haraka.
Makalla
aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi
Kata ya Uyole na kusema kufanya hivyo kutawafanya wananchi wazidi kuwa na imani
nao na serikali kwa ujumla.
Mkutano
huo wa hadhara ni muendelezo wa mikutano yake mbalimbali ya kusikiliza kero za
wananchi na kuzioatia ufumbuzi jambo ambalo linasaidia kuondoa malalamiko ya
wananchi.
“Watendaji
wa serikali tunapaswa kuwa wepesi na karibu na wananchi kila mahali ili kushughulikia
kero zao kwa haraka na kuwapa majibu mazuri,”alisema Makalla.
Alisema
zipo tabia za baadhi ya watendaji wa serikali ambao hutoa vitisho kwa wananchi
hivyo waache tabia hiyo na badala yake wafanye ofisi za serikali kimbilio la wananchi
ikiwemo kupunguza urasimu na lugha za maudhi kwa wananchi.
Katika
hatua nyingine ameuagiza Uongozi wa jiji la Mbeya kurejesha maeneo yote waliogawa
kwa raia wa kigeni ili taratibu zifuatwe na yarejeshwe kwa wananchi kwa ajili
ya soko.
Pia
ameagiza wananchi 36 waliotapeliwa
mashamba yao na mwekezaji warejeshewe baada ya mwekezaji kutokujenga
Shule kwa miaka 14 kama alivyoahidi.
Aidha
amewaagiza TRA kuweka utaratibu wa kwenda kwenye Kata kukusanya kodi ya majengo
badala ya kuwapa usumbufu wananchi kwenda kuweka foleni ofisi za TRA.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment