Watuhumiwa wa Ujangili, Peter
Kabi (wa pili kulia) na mke wake Leonida Loi Kabi (wa tatu kulia)
wakielekea kusomewa mashtaka ya kukutwa na meno 210 na mifupa mitano ya
tembo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo,
wote wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Mtuhumiwa wa Ujangili, Peter
Kabi (wa pili kulia) akielekea kusomewa mashtaka ya kukutwa na meno 210
na mifupa mitano ya tembo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini
Dar es Salaam leo, mtuhumiwa huyo na mke wake Leonida Loi Kabi (hayuko pichani) wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof.
Alexandre Songorwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari muda
mfupi baada ya hukumu hiyo leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo
anaeshuulikia Maendeleo ya Wanyamapori, Kanisius Karamaga.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof.
Alexandre Songorwa akizungumza na wanahabari katika moja ya ukumbi
mahakamani hapo.
*************
Na Hamza Temba -WMU
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela Peter
Kabi na Leonida Loi Kabi ambao ni wanandoa baada ya kukutwa na meno ya
tembo 210 yenye uzito wa kilo 450.6 pamoja na mifupa mitano ya tembo.
Meno
hayo yanayodaiwa kuwa ni sawa na idadi ya tembo 93 waliouwawa yalikutwa
nyumbani kwa washtakiwa hao tarehe 27 Oktoba, 2012 eneo la Kimara Stop
Over Jijini Dar es Salaam.
Hakimu
Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shahidi amesema ametoa hukumu hiyo
leo baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi wa upande wa Jamhuri
ukiongozwa na mawakili Paul Kadushi na Elia Athanas ambao kwa pamoja
umewatia hatiani washtakiwa hao.
Amesema
katika kosa la kwanza kila mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka 15
jela, kosa la pili na la tatu miaka 20 kila moja na kwamba hukumu hizo
zitaenda kwa pamoja.
Akitoa
ushahidi wa upande wa Jamhuri juu ya athari za ujangili nchini,
Mtaalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI),
aliyefahamika kwa jina moja la Lymo amesema idadi ya tembo hapa nchini
imepungua kwa kiasi kikubwa kwani sensa ya mwaka 2006 inaonyesha tembo
walikuwa 1,034,000 tofauti na sesa ya mwaka 2012 ambayo ilionesha idadi
hiyo kupungua na kufikia 43,000.
Alisema
sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya tembo kuongezeka na kufikia
50,000 ambayo ni matunda ya jitihada za Serikali katika kukabiliana na
ujangili kwa kuongeza nguvu katika doria na mikakati mbalimbali ya
kudhibiti ujangili.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya
Maliasili na Utalii, Prof. Alexandre Songorwa akizungumza na waandishi
wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo amesema, kila mtanzania
anapaswa kujifunza kupitia hukumu hiyo kwa kuwa binadamu wote hujifunza
kutokana na makosa na kwamba ni jukumu la kila mtanzania kulinda na
kuhifadhi rasilimali za taifa.
“Rasilimali
hizi ni zetu sote watanzania, sio za Serikali, sio za Wizara ya
Maliasili na Utalii, sisi ni vibarua wenu, tuwalindie watoto wetu na
wajukuu zetu hizi rasilimali, wasijekututukana huko mwishoni kama
hawatakuta chochote wakalazimika kupanda ndege kwenda kuangalia vitu
vilivyokuwa hapa hapa, watatutukana hatuna sababu ya kusubiri matusi”
alisema Songorwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment