Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca
Kwandu akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na
TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara,
Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali.
Mkuu
wa Kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo
ya Sekta ya Umma, Desderi Wengaa akizungumza na wajumbe wa kikao cha
mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa
ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa
mafunzo hayo leo Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza, Johnsen Bukwali katikati (walipokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya
mafunzo elekezi kwa Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Hallmashauri
na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kagera na Mara mara baada ya
kufungua mafunzo hayo leo Jijini Mwanza
****************
SERIKALI
imewataka Maafisa Habari na Maafisa Tehama katika sekretarieti za Mikoa
na Halmashauri za Wilaya nchini kuweka taarifa sahihi zenye kuzingatia
muda na wakati ili kuongeza ufanisi wa kutangaza shughuli za Serikali
kwa umma.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Mwanza na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Clodwig
Mtweve, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi, Johnsen
Bukwali wakati wa mafunzo elekezi ya uwekaji wa taarifa katika tovuti
yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Umma (PS3) kwa
Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga,
Mara, Kagera na Simiyu.
Kwa
Mujibu wa Mtweve alisema uwekaji taarifa katika tovuti hizo
zitasaidia kuimarisha shughuli za utawala na kuifanya Serikali
kufahamika zaidi kwa wadau wake na hivyo kupunguza malalamiko ya mara
kwa mara yanayotolewa na wananchi kuhusu huduma zake kwa umma.
“Ninyi
ndio mmekuwa wachakataji wa taarifa za Serikali na kuhakikisha
zinaufikia umma wa Watanzania zikiwa katika hali ya ubora kwa kutumia
njia mbali mbali za mawasiliano kama vile mbao za matangazo na hata kwa
njia ya mitandao” alisema Mtweve.
Kwa
mujibu wa Mtweve alisema kuwa lengo la Serikali ni kuongeza uwazi
na wigo wa upatikanaji wa taarifa sahihi na zenye uhakika katika tovuti
zake ili kuiepusha Serikali na habari za kuzusha na zisizo na maslahi
kwa taifa.
Aidha
Mtweve pia aliwataka Watendaji wa Serikali hao kuhakikisha kuwa
mafunzo hayo yanatoa fursa kwao katika kujibu maswali mbalimbali ya
wananchi yanayoulizwa kupitia mitandao ya kijamii na hivyo kuwawezesha
kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kutekelezwa katika Mikoa na
Halmashauri zao.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano katika Mradi wa
(PS3), Desderi Wengaa alisema mradi huo unatelezwa katika Mikoa 13 Bara
na Halmashauri 93 za Tanzania Bara, ambao katika awamu ya kwanza
itahusisha washiriki kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa pekee.
Aliitaja
mikoa inayotekeleza mradi huo kuwa ni Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera,
Rukwa, Mbeya, Iringa, Dodoma, Morogoro, Njombe, Mtwara, Kigoma na Lindi.
Wengaa
alisema mradi wa PS3 umejikita katika maeneo makuu manne ya utawala
bora, usimamizi wa rasilimali watu, rasilimali fedha pamoja na mfumo wa
mawasiliano ndani ya Serikali.
“Mafunzo
haya yamelenga kuwajengea uwezo Maafisa Habari na TEHAMA katika Mikoa
na Halmashauri kuweka taarifa katika tovuti zao ambazo zitasaidia
wananchi kufahamu kwa ukaribu zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Serikali katika maeneo yao” alisema Wengaa.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Rebecca Kwandu alisema ili mafunzo hayo yalete tija
iliyokusudiwa ni wajibu wa Maaafisa Habari na TEHAMA washirikiane kwa
karibu zaidi ili kuhakikisha taarifa taarifa muhimu zilizopo katika
maeneo yao ya kazi zinawafikia wananchi katika muda na wakati uliowekwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment