Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowasili wilayani Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakilakiwa kwa furaha walipowasili katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13,
2017.
Afisa
Ustawi wa Jamii Yeremia Ngoo akiwapa maelezo Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nyumbani kwa Bibi
Agnes Kamota (75) walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela
wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika
Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida
leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakitembelea Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13,
2017
Mke
wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi wakati yeye na
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli walipofanya ziara katika Makazi ya
Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo
Februari 13, 2017.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakishiriki kucheza ngoma na vikundi vilivyojitokeza kuwalaki katika
Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida
leo Februari 13, 2017.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi wakati yeye na mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13,
2017.
Waziri
Mkuu Mama Mary Majaliwa akihutubia wananchi wakati walipotembelea
Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida
leo Februari 13, 2017.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakioneshana kielele cha kilima cha Sukamahela ambapo inasemekana ndipo
ilipo alama ya kuonesha katikati ya nchi ya Tanzania wakati wa ziara yao
katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani
Singida leo Februari 13, 2017
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5 katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza
Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la
Benki ya NMB Singida Bw. Abius Mlengwa katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13,
2017.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakipokea msada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB
Manyoni Bw. Richard Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza
Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. PICHA
NA IKULU
**************
NA MWANDISHI MAALUM
MKE
wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu
Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia
watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.
Wake
hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika
vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na
wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.
Wameyasema
hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya
Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya
Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katika
kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele,
unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa
kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.
Akizungumza
na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka
eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na
hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.
Kwa
upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na
kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na
wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Watanzania
wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo
na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada
mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.
Awali
Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa
mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia
watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.
Bw.
Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja
huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na
zina nyufa.
Naye
Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana
aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa
kusaidia watu wasiojiweza.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment