Wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wakisubiria kupata Hati miliki zao
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akitoa hotuba yake wakati wa alipozindua utoaji wa Hatimiliki za kimila wilayani Mvomero
Mratibu wa Elimu kata ya Hembeti, Charles Kikully akisoma Risala ya vijiji vya Hembeti na Dihombo kwa Waziri Lukuvi
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Mohamed Utali akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Bw. Rugembe Maige akitoa taarifa ya wataalam ya Wilaya ya Mvomero na Tume ya Matumizi na Mipango ya Ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Dkt. Stephen Kebwe Akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa utoaji hati za Kimila. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi akiwatambulisha wageni walioongozana na Mh. waziri Lukuvi kwa wanakijiji wa Hembeti na Dihombo
Mwenyekiti wa Tume ya Mipango na matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akitoa neno la shukurani kwa Waziri Lukuvi kwa kuzindua rasmi utoaji wa Hakimiliki za Kimila, pia kutoa shukurani kwa viongozi mbalimbali, wadau na wananchi waliojumuika katika uzinduzi huo.
Wananchi mbalimbali wa Kijiji cha Hembeti na Dihombo wakikabidhiwa Hati za Kimila na Mh. Waziri Lukuvi
Baadhi ya wanakijiji wakisoma Hati zao
Wanakazi wa Mvomero pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo
Baadhi ya wanavijiji vya Hembeti na Dihombo wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Waziri Lukuvi mara Baada ya kumaliza zoezi la Ugawaji wa Hati hizo.
Picha na Fredy Njeje
Waziri wa Ardhi, nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William
Lukuvi,(MB) amezindua rasmi utoaji wa Hati Miliki za ardhi za Kimila
katika vijiji viwili vya Hembeti na Dihambo wilayani Mvomero mkoani
Morogoro ambapo amegawa hati 1361 baada
ya kupima vipande vya ardhi 2944.
Akizungumza na wanakijiji
hao Waziri Lukuvi alisema kuwa ameamua
kuja mwenyewe kuzindua ugawaji wa hati miliki ili apate kujiridhisha na kuona
kazi hiyo imefanyika kitimilifu na kutekelezwa kama alivyo agiza, alisema kazi
hiyo ni utekelezaji wa ilani ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) wa kuhakikisha nchi inapangwa kwa kupima ardhi yake ambapo
wananchi watapimiwa ardhi na kupewa hati
za kumiliki maeneo hayo, na kusisitiza kuwa baada ya kukabidhiwa Ardhi hiyo
ulinzi wa ardhi hiyo utakuwa ni juu ya mmiliki mwenyewe.
Alisema kuwa njia moja wapo ya
kuondoa migogoro ya ardhi ni kuhakikisha kuwa kila Mwanakijiji anamiliki kipande chake cha ardhi kwa kuwapatia hati za
kimila na kwamba pamoja na kugawa hati hizo bado wataalam watabaki kuendelea
kupima ardhi mpaka watakapo kamilisha zoezi hilo la kupima na kutoa hati za
vipande 5200 ambapo vijiji
vitakavyoendelea kupimwa ni pamoja na Hembeti, Ihombo,Bungoma,Kindo na
Kibugu pia kijiji cha Kambala ambacho nacho kipo tayari kwa ajili ya kuanza
kupimwa ambapo watapanga matumizi bora ya Ardhi na kutoa hati, ambapo matumizi
hayo ya ardhi yataainisha maeneo ya Kilimo na Ufugaji.
Na kwa maeneo ya kilimo
wafugaji hawataruhusiwa kulishia mifugo yao. Waziri Lukuvi amesisitiza katika
eneo la kambala watakapopima eneo la mifugo ni lazima wataalam waainishe na
idadi ya Mifugo watakao fugwa katika eneo hilo pamoja na kuweka miundombinu
kama josho la Kuogeshea na mabwawa ya kunyweshea maji ambapo wananchi nao watapaswa kuchangia
gharama kidogo ili kuepuka muingiliano baina yao na wakulima.
Waziri Lukuvi aliongeza kuwa
Wilaya ya Mvomero ndio Wilaya pekee nchini Tanzania ambayo Serikali imefanya
matumizi bora ya Ardhi kwa vijiji vingi zaidi kulipo wilaya yoyote Tanzania na
mpaka sasa yamefanyika matumizi bora ya
ardhi katika vijiji 73 Mvomero,na kusisitiza kuwa ardhi ya Mvomero bado ina
rutuba hivyo hawana sababu ya kungojea ruzuku ya mbolea kutoka serikalini. Pia
Waziri amewaonya madiwani wasigawe tena vijiji pindi uchaguzi unapokaribia kwa
kufanya hivyo watakuwa wameharibu utaratibu wa vijiji ambavyo tayari vimepimwa
kwa kuwa ugawaji huo hauwasaidii wananchi katika maendeleo bali huwanufaisha
wanasiasa wanaotaka vyeo.
Sambamba na hilo amewasihi waliopata hati hizo kuwa thamani yake ni kubwa zaidi
kulipo ardhi ambayo haijapimwa kwa kuwa kupitia ardhi hiyo mwanakijiji
anaweza kutumia hati hiyo kwa ajili ya kupata mkopo Benki, amewataka wale wanaokaidi
kushiriki katika zoezi za upimaji na matumizi ya ardhi na wao washiriki kwa
sababu mpango wa matumizi ya ardhi una faidia kubwa.
"Mpango huu wa upimaji
unaendelea wilaya za Kilombelo, Ulanga na Malindi ambapo watapanga kupima na
kutoa hati laki tatu (300,000) na kumalizia kuwa kila mtu ambaye amepewa hati
yake haruhusiwi kuiuza kwa mtu yoyote nje ya mwanafamilia wa kijiji ambapo
ndipo kuna mmiliki wa ardhi hiyo na
kuwasisitiza wale wote walio nje ya Mkoa wa Morogoro wafike pindi matumizi ya
ardhi na upimaji wanapofika katika maeneo yao." alisema Waziri Lukuvi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh.
Dkt. Stephen Kebwe akiongea na wanakijiji hao alisema kuwa mtu yeyote atakae
jaribu kuleta migogoro ya ardhi Serikali haita wafumbia macho na Sheria
itachukua mkondo wake kwa kuwa hao ndio wanaorudisha nyuma maendeleo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment