Kama
inavyojulikana kuwa Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2016 Jihan Dimack
aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi wa kumi na moja
mwaka 2016 aliondoka nchini tangu tarehe 11 Januari kuelekea Manilla
nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe kwa
ngazi ya kimataifa .
Jihan
Dimack akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni yupo
nchini Phillipines kwa muda wa wiki mbili sasa akiiwakilisha vyema
Tanzania katika kuwania taji hilo.
Mashindano
haya ambayo yanazingatia vigezo mbalimbali pia yana utaratibu wa
upigaji kura ambao umeshaziduliwa rasmi tangu tarehe 23 Januari 2017 na
kura zitapigwa ndani ya siku sita hadi tarehe 30 Januari 2017 ambayo ndo
finali za mashindano hayo.
Utaratibu
uliowekwa na uongozi wa Miss Universe mwaka huu ni kwamba kutakua na
warembo 12 bora na kati ya hao kumi na mbili mrembo mmoja ataingia kwa
kigezo cha kupata kura nyingi kupitia mtandoni.
Hivyo
basi Watanzania wote kwa pamoja tushirikiane katika hili kuhakikisha
mrembo wetu kutoka Tanzania Jihan Dimack anapata kura za kutosha
kumuwezesha kuingia katika fainali hizo.
Itakua
jambo la faraja sana kufanikisha ushindi kwa kutoa ushirikiano wa
kutosha kwa kupiga kura kwa wingi na kila mtu mmoja ana uwezo wa kupiga
mpaka kura kumi kwa siku. Ushindi wa mrembo wetu upo mikononi mwetu
wenyewe.
Ili uweze kumpigia kura mrembo wetu Jihan utatakiwa kufanya mambo machache yafuatayo:
Jinsi ya kumpigia kura Jihan katika mashindano ya Miss Universe kuanzia tarehe 23 January 2017:
1) VODI: Pakua Vodi app katika Google Store au Apple Store
2) Kupitia tovuti ya www.missuniverse.com
3) MISS U APP: Pakua Miss U app
4) TWITTER: Tweet kwa kutumia hashtag #MissUniverse alafu utatumia hashtag maalum ya Jihan itakayotolewa muda si mrefu.
Tafadhali kumbuka kwa kila mtu ataweza kupiga kura mara 10 kwa siku kwa kila akaunti aliyoisajili.
***Kumbuka kuwa website ya missuniverse.com ni mtandao pekee ambapo upigaji kura utaendeshwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment