Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akizungumza
na waandishi wa habari juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa
kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi
hiyo.Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu- Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Susan Mlawi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki na Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba
vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar
es Salaam wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi.
***************
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Angellah J. Kairuki
amezindua rasmi safari ya awamu ya kwanza kwa kuagamsafara wa magari yaliyobeba
vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi
huo Mhe. Kairuki alisema umefika wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari
ya kuamia makao makuu Dodoma ili kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya
kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
“Kufuatia agizo la Mheshimiwa
Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali
alihamia Dodoma Mwezi Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi
ya kutekeleza azma hii ya serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu
umma wa watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya
kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Aliongeza Mhe. Kairuki.
Amesema katika kundi la kwanza
jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara
ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi,
Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.
Katika hatua nyingine Mh.
Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na Waziri,Katibu Mkuu na Naibu
Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa masuala yote
yanayohusuu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma
kwa Ujumla yatatekelezwa Mjini Dodoma lakini.
Aidha masuala ya Mishahara,Uendelezaji
rasilimali watu,Ukuzaji maadili,Anuai za jamii,Uchambuzi ushauri na Utendaji
kazi na Huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano yataendelea
kushughulikiwa na ofisi ya Dar es Salaam.
Alisema Ofisi yake
itafunguliwa Rasmi Mjini Dodoma Tarehe 30 Januari 2017 na itakuwa katika Jengo
la College of Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha
Dodoma kama makao yake ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment