Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop, wakizindua rasmi awamu ya kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, Prof Richard Sigalla, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene .
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakipanda mti wa kumbukumbu.
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi huduma za kulipia usafiri wa mabasi ya mwendo kasi.
Rais John Magufuli akiingia katika kituo kwenda kupanda basi la mwendo kasi.
Rais Magufuli aliendesha kidogo moja ya mabasi hayo ya Mwendo wa haraka.
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakiteremka katika mabasi hayo ya mwendo wa haraka baada ya uzinduzi.
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop (kulia) na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi.
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakijadiliana jambo. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Wananchi mbalimbali wa Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo.
Wabunge na viongozi wa vyama nao walihudhuria.
Maofisa kutoka TAMISEMI nao walikuwepo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya makatibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam waliohudhuria.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop akizungumza na kutoa hotuba yake.
Msanii Banan Zoro akitumbuiza.
Mrisho Mpoto (kulia) na Banana Zoro wakitumbuiza kwa wimbo wa SIZONJE ambao unapedwa sana na Rais John Magufuli.
Mrisho Mpoto akighani mashairi ya Sizonje...
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, nae alikuwepo kushuhudia uzinduzi huo.
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakifurahia mashairi ya Sizonje. Kushoto ni Waziri Prof Makame Mbarawa.
Rais Magufuli alishindwa kujizuaia na kuamua kushuka kumtunza Mrisho Mpoto.
Wananchi wakimsikiliza Rais Magufuli aliyekuwa akihutubia.
Rais John Magufuli akihutubia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 25
Januari, 2017 amefungua rasmi awamu ya kwanza ya miundombinu na utoaji wa
huduma ya usafiri wa haraka wa mabasi (BRT) katika Jiji la Dar es Salaam
uliotekelezwa kwa lengo la kukabiliana na msongamano wa magari ndani ya Jiji na
athari zake katika shughuli za uzalishaji mali na ustawi wa jamii.
Mradi
huu wa kwanza kutekelezwa Afrika Mashariki na wa tatu Barani Afrika, umehusisha
ujenzi wa Kilometa 20.9 za barabara za Kimara – Kivukoni, Fire – Kariakoo na
Magomeni – Morocco, vituo vya mabasi 27, madaraja ya waenda kwa miguu 3 na
vituo vikuu 3.
Awamu
hii ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa miundombinu na utoaji huduma ya
usafiri wa haraka wa mabasi imegharimu Shilingi Bilioni 403.5 ambapo kati yake
Shilingi Bilioni 86.5 zimetolewa na Serikali ya Tanzania na Shilingi Bilioni
317 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Utekelezaji
wa mradi huu umepangwa kufanywa kwa awamu 6, naawamu ya pili ambayo ipo katika
maandalizi ya kumpata mkandarasi baada ya kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB), itahusisha ujenzi wa barabara ya kutoka katikati ya
Jiji – Mbagala, Magomeni – Chang’ombe na Chang’ombe – Jitegemee. Ujenzi huu
utahusisha jumla ya Kilometa 19.3 za barabara na barabara za juu 2 (Flyovers) katika eneo la Chang’ombe na
Uhasibu.
Akizungumza
kabla ya kufungua rasmi awamu ya kwanza ya mradi huu, Mhe. Rais Magufuli
amemshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kuanzisha mradi huo katika kipindi chake cha uongozi, na amewapongeza wadau
wote waliohusika katika utekelezaji ikiwemo Wizara ya Ujenzi na Benki ya Dunia iliyotoa
mkopo huo.
Mhe.
Rais Magufuli ameiomba Benki ya Dunia kuharakisha mchakato wa kutoa fedha za mkopo
utakaowezesha kuanza kwa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara
ya Ubungo (Ubungo Interchange) ili
kuongeza ufanisi wa mradi.
Mhe.
Dkt. Magufuli amesema nia ya Serikali yake ni kuifanya Dar es Salaam kuwa Jiji
la kisasa kwa kuhakikisha inakomesha tatizo la msongamano wa magari ambapo
pamoja na kutekeleza mradi huo pia itajenga reli ya kisasa (Standard Gauge) kati ya Dar es Salaam na
Morogoro na kujenga barabara za haraka (Express
Road) kati ya Dar es Salaam na Chalinze hivi karibuni.
“Tunataka
Dar es Salaam liwe Jiji la kisasa, ndugu zangu wa Dar es Salaam nataka mniamini
hivyo, hivi karibuni tunapitia tenda na tutapata Mkandarasi wa kuanza kujenga
reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo kuna jumla ya kilometa 200 na
treni zitakazopita zitatumia mafuta na umeme”
“Lakini
pia mchakato wa kujenga barabara ya haraka (Express Road) kutoka Dar es Salaam
hadi Chalinze yenye njia 6 na hatua zote zimekamilika na kilichobaki ni
mazungumzo na wakandarasi kabla ya kuanza kujenga”
amesema Rais Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli amezitaka mamlaka zinazohusika, kuhakikisha mradi huo unaendeshwa
kwa faida, miundombinu yake inatunzwa vizuri, wananchi wananufaika kama
ilivyokusudiwa na pia ametoa siku 5 kwa Jiji la Dar es Salaam kufanya uamuzi
juu ya matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 5.8 zilizotolewa na mbia
anayemiliki asilimia 51 ya hisa za kampuni ya UDA-RT.
Pamoja
na Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali na Viongozi wa vyama mbalimbali vya
siasa na sherehe hizo zimehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda
ya Afrika Bw. Makhtar Diop ambaye ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza mradi huu
muhimu kwa maendeleo na ustawi wa jamii na ameahidi kuwa
Benki hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa barabara zitakazosaidia kuondoa msongamano wa malori yanayokwenda
bandarini kupeleka na kuchukua mizigo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment