Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis
Juma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya
Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya
Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji
Ferdinandi Wambali (kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni
katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina
Revocati akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho
ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya
Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
***************
Benjamin Sawe, Maelezo.
Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika
viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kaimu Jaji Mkuu Prof.
Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali
ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa
miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa
uchumi.
Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi
maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja
Katika matembezi hayo Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi
maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea
maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.
Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa
ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma
mbalimbali za Kisheria
Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri
katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za
kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na
kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria
Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa
mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati
Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment