Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza
wakati alipoongoza kamati ya ulinzi na Usalama wilayani humo kuzungumza
na majirani zao waa Wilaya ya Mabanda mkoa wa Makamba nchini Burundi.
Kanali Gaguti akizungumza.
Ziara ikiendelea...
MKUU
wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma Kanali Marco Gaguti amewaonya
waomba hifadhi wenye historia ya uhalifu nchini Burundi wanaoingia
Nchini Tanzania kwa kigezo cha kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa kuhofia
wasikamatwe kwa uhalifu walioufanya Nchini mwao kuwa ikibainika hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha,
Gaguti aliuomba uongozi wa Nchi ya Burundi kutoa ushirikiano kwa vyombo
vya ulinzi na usalama vya Wilaya hiyo iliyopo Mpakani, kuweza
kuwabaini waomba hifadhi wanaoingia Nchini kwa kukimbia uhalifu
walioufanya Nchini mwao na kuja kuendeleza vitendo hivyo wanapo ingia
Nchini.
Hayo
yalibainika jana wakati wa Kikao cha majadiliano baina ya Mkuu huyo na
Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, alipokuwa
akihoji ni kwanini wahamiaji wengi wanaongezeka Nchini wakidai
wanakimbia vurugu zinazo endelea Nchini mwao ambapo kwa Mwezi january
waliingia waomba hifadhi 2230, ambapo ilibainika wengi wao wanadai
wanakimbia kukamatwa kwa kujihusisha na uhalifu na wengine kukimbia njaa
iliyopo majumbani kwao.
Gaguti
alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji wanaoingia Nchini
wakidai kukimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha Vijana wa chama
tawala kinacho julikana kama ( IMBONELAKULE) ambapo wanakuja kuomba
hifadhi katika Nchi ya Tanzania ilihali Nchi yao inaamani ya kutosha na
wengine kukimbilia kambini kuweza kupata hufuma za bure kwa kuhofia
njaa nchini mwao . Hali iliyopelekea Waziri wa Mambo ya ndani kusitisha
zoezi la Waomba hifadhi kuingia Nchini kwa kigezo cha kukimbia njaa
Nchini mwao na kukimbilia Tanzania iliwaweze kupata Msaada wa chakula ,
ni lazima Afanyiwe mahojiano na atoe sababu zilizo mfanya akimbie
iliaweze kupatiwa kibali cha kuwa mkimbizi.
Hata
hivyo Kanali Gaguti aliwaomba viongozi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo
vya ulinzi na usalama kuweza kuwabaini wahalifu hao waweze kurudisha
Nchini mwao na kuweza kuepukana na vitendo vinavyo endelea na ongezeko
la waomba hifadhi kuingia Nchini bila kufuata utaratibu.
''
leo nilikuwa natembelea vituo na kuona ongezeko ya wahamiaji lakini
serikali imetoa maelekezo mpya ikiwemo kuwatambua na kujua sababu za
kukimbia Nchini mwao lakini kama atakuwa na sababu za Msingi hata pata
fursa ya kuwa mkimbizi, lakini pia nikuombe ushirikiano kama kuna
taarifa za watu ambao ni wahalifu upewe taarifa mape ma kabla ya mambo
kubadilika Ile tuweze kuchukua tahadhari mape ma kwa panda zote mbili"
alisema kanali Gaguti.
Naye
mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba (Musitanteri)Niyonkuru
Laetitia alisema kwa sasa nchi ya Burundi ni tulivu na wanaokimbia
nchini mwao ni wale wanaokimbia njaa na wengine kukimbia uhalifu
aliofanya nchini Burundi na kuja Tanzania kuomba hifadhi.
Alisema
wengi waliofika Tanzania ni wale waliokimbia kwa mambo yao binafsi na
wengine ni wale wakimbizi waliorudishwa BUrundi kipindi cha nyuma
wanaokimbia wengi wanakuja kwa kigezo cha kupelekwa nje ya Nchi kama
vile America na Ulayana Nchi nyingine ilikuwafuata ndugu zao walio
pelekwa huko .
Aidha
aliuomba Uongozi wa Tanzania kabla ya kuwapokea wahamiahi hao kuchukua
vitambulisho vyao ilikubaini walio kimbia tuhuma zinazo wakabili, pia
kumekuwa na tetesi wengi wao wanaoingia kuomba hifadhi wanakuja
makambini kujifunza namna wanavyo weza kwenda kuipindua Nchi kwa
kupigana pindi wanapo wabaini waweze kuwakabidhi kwa Serikali ya
Burundi.
Kwa
upande wao baadhi ya Waomba hifadhi waliofika katika maeneo ya
kupokelea waomba hifadhi hao kwa mahojiano waweze kuingia kambini ,wengi
wao walidai wanakimbia vikundi vya IMBONELAKULE vinavyo wafuata
Nyumbani kwao usiku na kuwapiga na kuwatishia usalama wao hali inayo
walazimu kukimbilia Tanzania , suala lililo kanushwa na Mkuu wa Wilaya
ya Mabanda.
Nizigimana
Silivesta ni moja kati ya waomba hifadhi kutoka Burundi, alisema
kinacho wapelekea kukimbia Nchini mwao ni hali ya kiusalama kuwa ndogo
kumekuwa na tabia ya vikundi vya watu vinavyo wafuata kuwatisha kutokana
na baadhi ya ndugu zao walio kimbilia nchini kuwa wanamahusiano nao na
wanaipinga serikali.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment