Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam mbele ya Balozi wa India Bw. Sandeep Arya .
Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan picha mbali mbali zenye kuonyesha historia ya urafiki baina ya Tanzania na India wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi wa India jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akihutubia wakati wa uzinduzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini.
Vikundi vya Utamaduni wa Kihindi vikionyesha uwezo wa kuzicheza ngoma za asili.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ameishukuru
Serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika miji 17 nchi ambayo
inalenga kupunguza tatizo la maji kwa wananchi wengi nchini.
Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika
hafla ya Maadhimisho ya miaka 68 ya Siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya India sherehe
ambazo zimeambatana na Uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi mpya ya Ubalozi wa
India hapa nchini.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ufadhili wa miradi ya Maji pamoja na
miradi mingine unaofanywa na Serikali ya India kwa Tanzania Bara na Zanzibar
unadhihirisha wazi mahusiano mazuri yaliyopo yaliyoasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Mahatma Gandhi wa India.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa India ni moja ya washirika muhimu katika juhudi za kuwaletea
wananchi maendeleo na Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu katika maeneo
mengi ikiwemo ya kikanda na kimataifa kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande
Mbili yaani Tanzania na India.
Amesema kwa
miaka mingi sasa mahusiano ya kindugu yamekuwa yaakiimarika katika sekta
mbalimbali ikiwemo kisiasa,kidiplomasia, kibiashara, masuala ulinzi, utamaduni
na mwingiliano wa watu na watu.
Makamu wa
Rais pia ameishukuru Serikali ya India kwa msaada wake wa shilingi milioni 500
alioutoa kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera ambao walikubwa na tetemeko la ardhi mwaka
jana.
Ameeleza kuwa
Mahusiano kati ya India na Tanzania yamekuwa na manufaa makubwa ambapo idadi
kubwa ya watanzania wanaenda kupata mafunzo mbalimbali nchini India hasa
Madaktari na wamekuwa msaada mkubwa katika kuokoa maisha ya Watanzania.
Katika hafla
hiyo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hotuba yake alitoa salamu za
rambirambi kwa Serikali ya India kufuatia ajali ya treni iliyotokea katika
Jimbo la Andhra Pradesh na kusababisha vifo vya watu 30 na kujeruhi wengine.
“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kutoka salamu za Pole kwa familia za
wafiwa na majeruhi katika kipindi hiki kigumu kwa kumwomba Mwenyezi Mungu
azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi na tunawaombea majeruhi wapone
haraka. ’’
Kwa upande wake, Balozi wa India hapa nchini Sandeep
Arya amemhakikishia Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali ya India
itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kwa ajili ya manufaa
ya wananchi wa pande zote Mbili.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment