Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 10 August 2017

MANISPAA YA LINDI YAOMBA MAGHALA

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Kilimo walipomtembelea Ofisi kwake mjini Lindi kuangalia miradi inayoendeshwa kibiashara mkoani humo.



Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Kilimo walipomtembelea Ofisi kwake mjini Lindi kuangalia miradi inayoendeshwa kibiashara mkoani humo.



Maafisa kutoka Benki ya Kilimo wakifatilia kwa makini mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (hayupo pichani). Kulia ni Afisa Mikopo Mwandamizi, Mubezi Buberwa na Afisa Usimamizi wa Mikopo, Elizabeth Kitaluta (kushoto).



Meneja wa Mikopo wa TADB, Samuel Mshote akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (hayupo pichani) kuhusu fursa za mikopo inayotolewa na TADB.
                                                                        ***************
Na mwandishi wetu, Lindi
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kujenga na kuendeleza maghala ili kuwaweza wakulima wa manispaa hiyo kuhifadhi mazao yao.

Ndemanga amesema kuwa maghala ya kuhifadhi mazao yamekuwa ni eneo lenye changamoto kubwa hali inayorudisha nyuma tija kwa wakulima wa manispaa hiyo.

Akizungumza na ugeni kutoka TADB, uliongozwa na Meneja wa Mikopo wa Benki hiyo, Samuel Mshote, Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa kutokuwa na maghala ya kutosha katika  manispaa kumekuwa kikwazo kikuu kwa wakulima kufikia malengo yao kwa kuwa imekuwa ikiongoza gharama na upotevu mkubwa wa mazao yao.

“Changamoto ya uhaba wa maghala imesababisha manispaa kutokupata mapato stahiki kwa kuwa uhifadhi wa mazao umekuwa ukifanyika katika maghala ya watu binafsi ambayo hayakidhi mahitaji halisi ya manispaa,” alisema Ndemanga.

Aliongeza kuwa ujio wa Benki ya Kilimo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto hiyo.

Naye, Meneja wa Mikopo wa Benki hiyo, Samuel Mshote alisema kwa kutambua changamoto zinazowakabili wakulima Benki ya Kilimo imeandaa mikopo maalumu kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ikiwemo ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao.

“Mikopo hii ni kwa ajili ya kujengea miundombinu ya aina mbalimbali kwenye mlolongo wa thamani, kwa mfano: skimu/ mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji mengine ya miundombinu za kilimo,”alisema Mshote.

Kwa mujibu wa Mshote, mikopo ya aina hii itarejeshwa kwa awamu katika kipindi cha miaka 5 hadi 15.

Akifafanua zaidi Mshote alisema kuwa ukokotoaji wa marejesho huendana na uwezo wa kuilipa kwa kuzingatia mpango kazi, na hivyo kipindi kilichoridhiwa kwenye mkataba.

“Tunatambua kuwa miundombinu ya aina hii, mara nyingi thamani yake huongezeka kadiri muda unavyopita, miundombinu hiyo huhitaji uangalizi mzuri (maintenance),” alisema.   


Wednesday, 9 August 2017

KILOLO DC YASHIKA NAFASI YA TATU KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Mgeni rasmi katika kilele cha Maonyesho haya alikuwa waziri wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za Mitaa MHE. George B. Simbachawene akimkabidhi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah tuzo ya mshindi wa tatu sambamba na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Aloyce Kwezi.Katikati DC wa kilolo Asia Abdallah , kushoto aliyeshika hati, Mkurugenzi Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi na mwishoni kwa Mkurugenzi ni Dkt. Mwingira Afisa Mifugo mkuu Wilaya na kulia tena huku ni Afisa Kilimo mkuu Wilaya ndgu. Kuziwa.
Na Fredy Mgunda, Mbeya
Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani iringa imeshika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane ambao huhusisha maswala ya kilimo yaliyofanyikia jijini mbeya kwa kanda ya nyanda za juu kusini na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka mikoa yote ya nyanda za juu kusini.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo ya nane nane  mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliwapongeza wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Kilolo Kilimo kinasaidia kuinua kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Mimi niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya ya Kilolo maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote za nyanda za juu kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu"alisema Abdallah

Abdallah alisema kuwa atakaa na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza na kuwa wilaya ya mfano huku nyanda za juu kusini hata Tanzania kwa ujumla.

"Sasa kazi imeanza na nitahakikisha kila kitu mwakani kitakuwa vizuri na tutafanya vizuri sana kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na ufugaji hivyo lazima tutatafuta njia mbada ya kuinua Kilimo cha wilaya ya Kilolo" alisema Abdallah

Aidha Abdallah alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.

"Mikakati iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie ushindi mnono zaidi" alisema Abdallah


Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Aloyce Kwezi alisema kuwa halmashauri inamikakati mingi ya kuboresha maeneo ya Kilimo kuwaomba wadau mbali mbali wanaotaka kuwekeza kwenye Kilimo wafike katika ofisi halmashauri ili kujadiliana namna ya uwezaji na maeneo wanayoweza kuwekeza.

"Halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri kwa ajili ya Kilimo ambayo bado hayafanyiwa Kilimo hivyo naomba wadau wenye nia ya kuwekeza kwenye Kilimo waje kuweza maana maeneo ni rafiki kwa Kilimo cha aina yoyote ile kutokana na hali ya hewa iliyopo huku" alisema Kwezi

Naye afisa mifugo mkuu wa wilaya ya kilolo Dkt. Mwingira aliupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo kwa jitihada za kuinua Kilimo na ufugaji kwa wananchi wa Wilaya hiyo na ndio sababu kubwa kupata mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane.

"Mimi nampongeza sana Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa ubunifu wao ambao umetusaidia kufika hapa hivyo naomba tuwape ushirikiano katika kukuza Kilimo cha Wilaya ya Kilolo "alisema Dr mwingira

Katika maonyesho hayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa George Simbachawene na huku nafasi ya kwanza ilichukuliwa na halmashauri ya Mpanda na nafasi ya pili ilishikwa na Tunduru.


Tuesday, 8 August 2017

MAJI SASA KUUNGANISHWA KWA NJIA YA SIMU

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akifafanua jambo kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa mawasiliano katika simu za mikononi inayowawezesha kupata taarifa zote muhimu za shirika hil kwenye simu. Pamoja naye ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro.
KATIKA kuhakikisha inarahisisha upatikanaji wa  huduma ya majisafi na kwenda na mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kiteknolojia, Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezindua mfumo mpya wa mawasiliano ambao unalenga kumrahisishia mteja kupata na kutoa taarifa zinazohusu huduma hiyo kwa haraka zaidi.

Huduma hiyo mpya sasa itapatikana kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) wa DAWASCO, Kiula Kingu amesema lengo kuu la mfumo huu ni kumweka mteja karibu kihuduma na kila mwananchi ana uwezo wa kutumia mfumo huo katika simu yake kupitia mitandao yote ya simu za mikononi nchini.

Kingu ameongeza kuwa ili mteja kunufaika na mfumo huu anatakiwa kuhakikisha ana simu ya mkononi ya “Smartphone” ambayo itamwezesha kupakua mfumo huo mpya wa DAWASCO, kisha kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajili mteja atatumiwa neno la siri ambalo litamwezesha kuingia na kupata taarifa husika. “Sisi Dawasco tumeona haja ya kujiboresha na kwenda sawa na teknolojia kwa kumletea mteja wetu mfumo rahisi ambao utamwezesha kupata taarifa zetu kupitia simu yake ya mkononi muda wowote,”alisema Bw. Kingu.

Naye, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji  ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.

“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Lyaro.

Anasema kwa sasa wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO itatumia taarifa hizo kumtafuta mteja na kukamilisha taratibu nyingine hadi kuhakikisha mteja anapata huduma ya maji.

 Katika kutimiza agizo la Waziri wa Maji na Imwagiliaji, Mhandisi Greyson Lwengwe la kuhakikisha wakazi wa Dar es salaama, Miji ya Kibaha na Bagamoyo wanapata  huduma ya maji safi, DAWASCO imekua ikijitahidi kuwafikia wananchi kwa njia na mbinu tofauti, kampeni tofauti kama 'mama tua ndoo ya maji kichwani' huku maunganisho ya maji kwa mkopo yakisaidia upatikanaji na uboreshaji wa huduma ya maji kwa maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam.

Mpaka sasa takribani watumiaji 25,000 wa mitandao ya simu jijini Dar es Salaam wameshapakua mfumo huu na lengo la DAWASCO ni kuwafikia wakazi wengi zaidi kwa kipindi kifupi. 


KAMPENI UCHAGUZI TFF ZAENDELEA, WALIOKATWA WAREJESHWA

Kampeni za wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika shirikisho, zinaendelea.

Kwa mujibu wa kanuni 11.10 ya uchagizi wa TFF, kampeni hizo za wiki moja hadi Ijumaa wiki hii ambako Uchaguzi Mkuu utafanyika Agosti 12, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Mtakatifu Gasper mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa kamati hiyo iliyokutana Jumamosi Agosti 5 2017, wagombea ambao wanawania urais ni pamoja na  Wallace Karia, Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais wanaowania ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.

Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro Samson wakati Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza wamo Aaron Nyanda, Vedastus Lufano, Samwel Daniel na Ephraim Majinge.

Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) wanaowania nafasi hiyo ni Stanslaus Nyongo, Bannista Rogora na Mbasha Matutu ilihali Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na Peter Temu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


FUATILIA UCHAGUZI WA KENYA HAPA MBASHARA


RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TANO MKOANI TANGA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzirasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji wa Korogwe mkoani Tanga katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzirasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji wa Korogwe mkoani Tanga katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017 BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


Sunday, 6 August 2017

MAKONDA, RUGE NA KUNDI LA TANZANIA ALL STARS WANOGESHA UZWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA HOIMA -TANGA

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars baada ya Rais John Magufuli kuwaambia wamalize tofauti zao. Ruge ndiye alimfuata jukwaani Makonda ili wajumuike na wasanii hao kucheza nao.
 Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakijiandaa kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Wasanii nyota wa filamu wa Bongo Movie wakiwa  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wamalize tofauti zao na kuweka maslahi ya nchi mbele wakati alipohutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Baada ya kupatanishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba walishuka jukwaani bega kwa bega huku wakitabasamu. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


Saturday, 5 August 2017

MAPOKEZI YA RAIS MAGUFULI MKOANI TANGA

 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea mkoani Tanga ambako katika ziara yake ya siku tano ataungana na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kesho Jumamosi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima hadi bandari ya Tanga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  maelfu ya wananchi wa Mkata  akiwasili mkoani Tanga. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


Friday, 4 August 2017

MAKONDA APOKEA VITANDA 150 VYA HOSPITALI NA MAGODORO YAKE KUTOKA AMSONS GROUP

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijaribu moja ya vitanda 150 alivyopokea msaada kutoka  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Samaam Paul Makonda, (kulia) akipokea msaada  wa Vitanda 150 na magodoro 150 pamoja na mashuka vyenye dhamani ya shilingi milioni 300, kwa Meneja Biashara wa Kampuni ya Mafuta Camel Oil, Suleiman Amour. makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye tamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.

Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

“Sitaacha kutafuta kwaajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri ili siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Magufuli, sisi tunataka Maendeleo na sio Siasa ndio maana hivi vitu vyote tunavyofanya vinatumiwa pia na wapinzani” Alisema Makonda.

Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kinamama watatu hadi wanne.