Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya
Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye ukumbi wa
Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa, Makame Mbarawa mashine 10 za kufyatua
matofali alizokabidhiwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi kabla ya kufungua semina ya Bodi hiyo kwenye ukumbi
wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018. Mashine hizo zitagawiwa bure kwa
vikundi vinavyojishugulisha na ufyatuaji matofali. Watatu kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na wanne kuil ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Joseph
Nyamhanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mauzo wa
Kampuni ya Locks and Systems Limited ya Dar es salaam, Linda Mwamukonda
kuhusu vitasa, bawaba na milango ya kielektroniki wakati alipotembelea
banda la kampuni hiyo katika maonesho yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili
wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye viwanja vya Hazina
jijini Dodoma, Mei 18, 2018.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua
Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.
Baadhi ya washiriki wa Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya
Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua semina hiyo kwenye ukumbi wa
Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ngao ya shukurani kutoka
kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji
Majenzi, Dkt. Ludigija Boniface Bulamile baada ya kufungua semina
Endelevu ya 29 ya Bodi hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei
18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi
walioshiriki katika Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa
Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi baada ya kufungua semina hiyo
kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018. Kutoka kushoto ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa, Makame Mbarawa,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi, Joseph Nyamhanga na Mwenyekiti wa
Bodi ya Usajili wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dkt.
Ludigija Boniface Butamile.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment