Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) akipokea Mwenge wa Uhuru baada ya
kuwasili kwenye jimbo lake la Muhambwe Wilayani Kibondo mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akishiriki uzinduzi wa
Kituo cha Afya cha Mabamba kilichopo kwenye jimbo lake la Muhambwe wakati wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru za kitaifa uliofanyiwa na kiongozi wa kitaifa wa mbio
hizo Bwana Charles Kabeho (wa tatu kushoto) kwenye kata ya Mabamba wilayani
Kibondo, Kigoma
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Loyce Bura (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Woilaya ya Kakonko, Kanali Hossea Ndagala kwenye
kijiji cha Mkubwa kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Kibondo na Kakonko.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akigawa chandarua kwa wanawake wenye
watoto baada ya uzinduzi wa kituo cha Afya cha Mabamba kilichopo kwenye jimbo
lake la Muhambwe wilayani Kibondo, Kigoma wakati wa mbio za Mwenge wa uhuru za
kitaifa
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, Mbunge wa jimbo la Muhambwe wilayani
Kibondo, Kigoma akipiga ngoma kuburudisha wapiga kura wake wakati wa kupokea
mbio za Mwenge wa Uhuru za kitaifa uliowasili kwenye Wilaya hiyo.
Hayo yameelezwa na
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) wakati
akipokea mbio za mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilaya ya Kibondo kwenye jimbo
lake la Muhambwe ukitokea Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma. Amesema kuwa Wilaya
ya Kibondo imeongoza kwa ufaulu wa shule za sekondari kwa miaka miwili
mfululizo ya masomo mwaka 2016 na 2017 ambapo kidato cha pili wameshika nafasi
ya nane kitaifa na kidato cha nne wameshika nafasi ya tisa kitaifa na kuzibwaga
sekondari nyingine zilizopo kwenye jumla ya Wilaya 187 nchini.
Nditiye amefafanua
kuwa shule hizo zimezawadiwa kiasi cha shilingi milioni 680 na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kupitia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (E4P) ambao umeleta
chachu, ari na ushindani kwenye kiwango cha ufaulu kwenye shule mbalimbali
nchini. Amefafanua kuwa fedha hizo zimetumika kugharamia upatikanaji wa
miundombinu mbalimbali kwenye shule ya sekondari ya Malagarasi na ya Wasichana
ya Kibondo.
Ameongeza kuwa ushindi
huo umeleta chachu na mwamko zaidi kwa wanafunzi, walimu, wazazi, walezi na
wadau wa elimu kwenye Wilaya hiyo ambapo wamejipanga kuchangia ujenzi wa
miundombinu mbali mbali kwenye shule za Wilaya hiyo ili kuongeza ufaulu kwa
wanafunzi ambapo imeendana na kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu
isemayo, “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwenye Elimu kwa Maendeleo ya
Taifa”.
Mhandisi Nditiye
amesema kuwa Wilaya ya Kibondo inaunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muunano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kutoa elimu bure nchini kote
kwa shule za msingi na sekondari ambapo wazazi hawalipi ada yeyote hivyo
inawawezesha kushirikiana kuendeleza miundombinu ya shule na mahitaji ya huduma
nyingine ili wanafunzi waweze kujisomea na hivyo kuongeza ufaulu wao.
Naye kiongozi wa
kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu Bwana Charles Kabeho amewataka
wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanamuunga mkono Mhe.
Rais wa nchini yetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata
sare za shule, vitabu vya masomo mbali mbali na miundombinu mingine ili
kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa manufaa ya wanafunzi na
walimu.
Amefafanua kuwa azma
ya Dkt. Magufuli ni kuwa na nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ambapo
haya yote hayawezekani pasipo kuwa na taifa lenye rasilimali watu yenye elimu,
ujuzi na maarifa ya kuendesha na kusimamia viwanda vyetu.
Bwana Kabeho
amemshukuru na kumpongeza Mhandisi Nditiye kwa kutambua umuhimu wa mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa na kujumuika na wananchi wa jimbo lake la Muhambwe
lililopo kwenye Wilaya ya Kibondo. “Mheshimiwa Nditiye, natambua majukumu
uliyonayo katika kipindi hiki cha Bunge la bajeti ambalo linaendelea mkoani
Dodoma lakini umejali na kuja kujumuika nasi katika kuzindua miradi mbali mbali
ya maendeleo kwenye Wilaya hii,” amesema Kabeho.
Mbio za Mwenge wa
Uhuru kitaifa zimepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mheshimiwa Loyce Bura
kwenye kijiji cha Mkubwa mpakani mwa Wilaya ya Kibondo ukitokea kwenye Wilaya
ya Kakonko. Mwenge umetembezwa kwenye Wilaya ya Kibondo na kuzindua miradi
mbali mbali ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya shilingi 1,512,000,000
ikiwemo kituo cha Afya cha Mabamba, kiwanda cha kusindika na kuzalisha unga wa
muhogo, ofisi ya ushauri wa kibiashara, hoteli na kugawa asiimia kumi ya mapato
ya Halmashauri hiyo kwa vikundi vya waasiriamali wanawake, vijana na walemavu
kiasi cha shilingi milioni 58.
Mwenge umekabidhiwa
kwenye Wilaya ya Kasulu ili kuendelea na mbio zake na kuzindua miradi mbali
mbali ya maendeleo nchini ambapo makabidhiano hayo yamefanyika kwenye kijiji
cha Mvugwe mpakani mwa Wilaya ya Kibondo na Kasulu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment