Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) watashirikiana
kwa pamoja kuandaa Maonesho ya Kilimo NaneNane Kitaifa yatakayofanyika Mkoa wa Simiyu Mwaka 2018.
Akiongea na waandishi
wa habari Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utatoa
dira ya kuyafanya Maonesho ya Kilimo NaneNane yawe ni Maonesho ya Kilimo
Biashara ili Watanzania wapate fursa ya kuona teknolojia mbalimbali kwenye eneo
la kilimo, mifugo na uvuvi.
“Matarajio yetu kama
mkoa kwa kushirikiana na TanTrade ni kuona kwamba tunaingiza Maonesho ya Kilimo
NaneNane kuwa tukio ambalo litawakaribisha watu wenye teknolojia mbalimbali
Kitaifa na Kimataifa kwenye kuwezesha mageuzi ya kilimo,uvuvi na ufugaji wa
nchi kwa kuonesha ni kwa namna gani wanaweza kumfikia mkulima, mvuvi na mfugaji
mdogomdogo kwenye teknolojia ya kisasa ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili
Maonesho ya Kilimo NaneNane yawekwe kwenye ramani ya dunia” alieleza Mtaka
Aliendelea kwa
kuziomba Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali kuyatumia Maonesho haya
kuyatangaza kwa kukaribisha makampuni yenye teknolojia kuja kuonesha mkoani
Simiyu.
Mtaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwa makundi yote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika eneo litakalofanyika Maonesho ya Kilimo Biashara ili uwekezaji huo uendane na viwango vya Kimataifa.
Mtaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwa makundi yote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika eneo litakalofanyika Maonesho ya Kilimo Biashara ili uwekezaji huo uendane na viwango vya Kimataifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka ameeleza
kuwa TanTrade ni taasisi pekee iliyopewa jukumu la kusimamia masuala ya Maonesho
ndani na nje ya nchi kisheria.
Hivyo,Rutageruka amesema kutokana na
uzoefu wa uandaaji wa Maonesho mbalimbali,
kwa mwaka 2018 Maonesho ya Kilimo Biashara yatakuwa ni Maonesho bora
kwasababu watawaandaa washiriki wote Kisekta, kuweka miundo mbinu ya kisasa na kuyafanya
Maonesho haya kuwa ya Kimataifa.
“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu ina kiu ya kuona Maonesho ya Kilimo Biashara yanakuwa ya kisasa kama ilivyo Maonesho ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam ambayo kwa Afrika Mashariki ndio Maonesho yanayoongoza kwa
ubora na Maonesho haya ya Kilimo tutayafikisha huko” aliongeza Bw Rutageruka
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment