Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Nzega vijijni, Hamisi Kigwangala akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi pikipiki 19 kwa watendaji wa Vijiji jimboni humo.
Makabidhiano ya pikipiki hizo
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Nzega Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa chama hicho taifa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza
Shughuli za chama.
JIMBONI NZEGA Jana, tulikabidhi pikipiki 19 kwa Kata zote 19 za jimbo la Nzega Vijijini. Hizi ni jitihada zetu katika kuimarisha Chama ngazi ya kata kwenye jimbo letu. Tulifanya zoezi hili mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo la Nzega Vijijini ambapo Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana aliitikia ombi letu la kuwa mgeni rasmi.
Chama cha mapinduzi kimejengwa kwenye msingi imara wa wanachama wenyewe kujitoa na kujitolea kukiimarisha. Hiki ni Chama cha watu, cha wanachama wenyewe. Viongozi wa Chama tunakiimarisha Chama chetu kwa kujitoa kama hivi.
Viongozi wote wa Chama hiki hatuna mishahara, walau baadhi yetu tunapata posho kidogo wakati wa kutekeleza majukumu yetu. Kwa kule ngazi za chini kuna watu wanajitoa kwa nguvu zao zote, kila kukicha, tena bila mshahara wala posho. Wanazunguka kijiji kwa kijiji, mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, kwa nguvu zao, kwa gharama zao na wakati mwingine huhatarisha maisha yao.
Binafsi naithamini sana kazi ya viongozi wenzetu kule chini kwenye grassroots, wanafanya kazi kubwa. Kongole kwao.
Wanafanya Kazi hii kuiweka CCM madarakani ili kuhakikisha amani, utulivu na usalama unadumu nchini. Kazi yao inatoa fursa ya shughuli za maendeleo ya nchi yetu kufanyika. Hawa ni Askari wazalendo kweli kweli! Kazi yao ni yenye heshima kubwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment