Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 23 September 2017

TIMU YA VIONGOZI MKOA WA MBEYA YAANZA KUJIFUA

TIMU ya soka ya Viongozi Club ya mkoa wa Mbeya chini ya Kocha Mchezaji Amos Makalla imeanza kujifua kwaajili ya michezo mbalimbali.

Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo, Kocha wa Timu ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema timu hiyo imepata mialiko mingi ikiwepo ule wa Bunge Sports Club na timu za Veterans za mikoa ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Katika mchezo wake wa mwisho, timu ya Viongozi mkoa wa Mbeya ilishinda kwa bao 4-1 dhidi ya timu ya Viongozi wa Dini.

Makalla alisema timu hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha mazoezi kwa viongozi na kuonesha mfano wa uongozi wa vitendo katika kuhamasisha michezo katika jamii.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment