WABUNGE wa Bunge la Canada ambao pia ni
wanachama wa Mabunge ya Jumuia ya Madola
kupitia Mwenyekiti wao Yasmin Rantasi wamepongeza utendaji kazi wa Rais
John Magufuli.
Wabunge hao waliopo katika ziara ya kikazi
nchini waliyasema hayo wakati wa kikao maalum baina ya Wabunge hao na
Mwenyekiti wa Mabunge ya Jumuia ya Madola Tawi la Tanzania, Dk Raphael Chegeni pamoja
na ujumbe wa Bunge la Tanzania, mkutano uliofanyika Ofisi ndogo za Bunge jijini
Dar es Salaam.
“Tumefurahishwa sana utendaji kazi wa serkali ya
awamu ya tano chini ya Rais Dk. John
Magufuli….Uwajibikaji ndani ya serkali umeongezeka, kubana matumizi, vita dhidi
ya rushwa na uwekaji wa misingi ya uchumi ni ishara tosha kuwa Tanzania
itafanikiwa kukuza uchumi na kupunguza kiwango cha umaskini pamoja na kuboresha
huduma za kijamii kwa muda mfupi,” alisema Rantasi.
Rantasi alisema kuwa yeye alizaliwa hapa Tanzania
enzi za utawaka wa Mwl. Julius Nyerere na kuondoka akiwa mdogo hivyo kurudi
tena katika ardhi hii na kuona maendeleo yanayofikiwa vinampa faraja.
Ujumbe huo unafanya ziara kwa nchi tatu za Afrika
zikiwemo Ethiopia, Tanzania na Zambia.
Aidha katika mkutano huo, Dk Chegeni aliwataka
wabunge hao kujikita zaidi katika masuala ya kibunge na hasa shughuli na majukumu
ya kimsingi ya kibunge ambayo ni
utungaji wa sheria, uwakilishi na usimamizi na ushauri wa serkali zao.
Alisema tawi la Canada lina nafasi kubwa la
kuyasaidia matawi mengine ya kibunge kutambua majukumu yakiwemo masuala ya
demokrasia, kufuata sheria na kuheshimu utawala wa katiba zao, pia kutambua utenganifu wa mihimili ya dola.
Katika hatua nyingine, Wabunge hao wamekubali
kuanzisha ushirikiano wa kibunge wa moja kwa moja na Bunge la Tanzania ikiwa
pamoja na kubadilishana uzoefu, kutembeleana na pia kuhamasisha ushirikiano wa
karibu wa serkali hizi mbili.
Pamoja na kikao hicho Dr. Chegeni alisisitiza
kuwa hapa Tanzania hakuna raia aliye juu
ya sheria hivyo kila raia anapaswa kuheshimu na kutii sheria ambazo bunge
linazitunga.
Sambamba na hilo aliwakumbusha wabunge hao
kuendelea kuelimisha wabunge wengine kwa kutumia uzoefu wao na wa mabunge yao
njia sahihi za kuheshimu mihili mingine.
“Lengo kuu la wananchi wa Tanzania ni kuendelea
kushirikiana na waCanada kupitia serkali zetu ili kuboresha ustawi wa jamii
pamoja na kukuza uchumi kwa faida ya watu wa pande zote,”alisema Dk.Chegeni.
Chegeni ambaye pia ni Mbunge wa Busega, mkoani
Simiyu aliwataka wabunge hao kuwahimiza wananchi nchini Canada kutumia vyema
rasilimali zilizopo nchini katika uwekezaji kwakua nchi hiyo imejaaliwa
teknolojia za kisasa na mitaji ya kutosha.
Rantasi alisema wataendelea kuishauri serkali
yao ya Canada izidi kuongeza misaada na kuimarisha uhusiano baina ya serikali
hizo mbili kwa maslahi mapana ya mataifa hayo.
Pia walimhakikishia Dk Chegeni kuendelea
kushawishi wananchi na makampuni yao kuendelea kutumia fursa za uwekezaji
zilizopo hapa nchini kuwekeza zaidi kwani wanaamini Tanzania bado ni nchi yenye
utulivu wa kisiasa, inafuata utawala wa sheria na watu wake ni wakarimu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment