MCHEZAJI wa Kimataifa mwenye mafanikio ya marakwa mara kila ajiungapo na Wenkundu wa Msimbazi Simba, Emmanuel Okwi leo ameibuka nyota wa mchezo wa kwanza wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani baada ya kutikisa nyavu mara nne simba ikishinda 7-0.
Okwi alidhihirisha umwamba wake huo baada ya kuiwezesha timu yake kupata ushindi mnono huo wa mabao ambapo hadi kipindi cha kwanza kinaisha alisha fumania nyavu mara 3, huku Shiza Kichuya, Juma Luzio na Erasto Nyoni wakiwa wametikisa nyavu mara moja kila mmoja kwa nyakati tofauti za mchezo.
Okwi akimpongeza Shiza Ramadhani Kichuya kwa kupachika bao.
Erasto nyoni wa Simba akifukuzia mpira
Ufundi ndio kitu walicho jaaliwa wachezaji wengi wa Simba kama hapa anavyoonesha.
Erasto Nyoni akipongezwa kwa kufunga bao.
Ruvu Shooting walishindwa kujielewa na hata ilifika wakati mlinda mlango wao kutakaa mabadiliko langoni.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
Mashabiki na wapenzi wa Simba wakifuatilia mtanange huo.
Waziri wa zamani Othman Juma Kapuya ni miongoni mwa mashabiki na wapenzi wakubwa wa Simba, hapa akiwa Uwanjani na aliyepata kuwa Mbunge wa zamani wa Lindi Mjini, Mohamed Abdul Azizi na kwambaali nyuma ni Mbunge wa Chalinze ambaye ni mnazi wa Yanga, Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya naye alikuwepo kushuhudia Simba ikivunja vunja bunduki za Jeshi
Mashabiki wakiwa na watoto wao Uwanjani.
Ni shangwe tu kwa wana Msimbazi
Okwi akishangilia bao lake la 4 na la sita kwa Simba.
Erasto Nyoni nae alikuwa akihama na kijiji
Ni kuoneshana ufundi tu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment